HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2019

JESHI LA POLISI MBEYA LAHAHA KUWASAKA WALIOMTEKA NA KUMTESA MDUDE CHADEMA

Kushoto Mdude Chadema akiwa hoi kwa kipigo baada ya kuokotwa alipotelekezwa na watu wasiojulikana. Katikati na kulia kabla ya tukio hilo.
Mdude Chadema.
Mdude Chadema akiwa wodini anakopatiwa matibabu.


NA MWANDISHI WETU, MBEYA
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, limesema linaendelea na upelelezi na msako mkali kuwasaka waliohusika na tukio la kutekwa, kuteswa kisha kutelekezwa kwa Mwanaharakati wa Chadema, Mdude Mpaluke Nyagali maarufu kama Mdude Chadema, aliyepatikana juzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, iliyotolewa leo Mei 10, Polisi Mbeya imekiri kuwa Mdude Chadema aliokotwa usiku wa saa 3, huko Inyala katika Kijiji cha Mtakuja kilichopo mkoani Mbeya, siku nne baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.

“Mnamo Mei 04, 2019 majira kati ya saa 1:00 na 2:00 usiku, huko Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe, mtu mmoja aitwaye MDUDE MPALUKE NYAGALI (31), ilibainika kuwa amechukuliwa na watu ambao hakuweza kuwatambua na kupelekwa mahali pasipojulikana.

Taarifa zilifikishwa Polisi mkoa wa Songwe na ufuatiliaji ulianza mara moja na mnamo tarehe 08 Mei, 2019 majira ya saa 3:00 usiku, huko Inyala katika Kijiji cha Mtakuja kilichopo mkoa wa Mbeya, alionekana mtu anaomba msaada.

“Ndipo dereva wa pikipiki ‘bodaboda’ aitwaye EMMANUEL KANAMGONDE na mwenzake AYUB WILSON, walimbeba na pikipiki hadi kwa uongozi wa Serikali wa Kijiji cha Mtakuja,” imesema taarifa ya Jeshi la Polisi Mbeya na kuongeza;

“Mhanga wa tukio hili baada ya kufikishwa kwa viongozi wa kijiji hicho, alijitambulisha kuwa yeye anaitwa MDUDE MPALUKE NYAGALI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na akaomba wajulishwe viongozi wake.

“Kisha mhanga alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili,” imemaliza taarifa ya Jeshi la Polisi Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Pages