HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2019

Majaliwa aipongeza Total kuchangia uchumi Tanzania

 Baadhi ya wageni wakiwa katika jubilee ya miaka 50 ya Kampuni ya Total.
 Meza Kuu.
Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman, akizungumza na jambo naWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
 Sehemu ya wageni waalikwa.
Kikundi cha ngoma cha Mama Afrika kikitumbuiza.
Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal, akitoa hotuba yake.
Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman, akitoa hotuba yake. 
 Baadhi uya viongozi wa Tatol wakisikiliza hotuba ya Wazirri Mkuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kinyago cha zawadi kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kinyago cha zawadi kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kinyago cha zawadi kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman.
 Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Total Tanzania akipokea zawadi ya cheti kwa kutambua mchango wake kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.




 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata keki katika hafla ya jubilee ya miaka 50 ya Total Tanzania.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman wakipiga makofi.
Picha ya Pamoja. 


NA SALUM MKANDEMBA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Total kwa mchango mkubwa inayotoa katika uchumi wa Tanzania, kupitia Sekta ya Mafuta, ikiwemo ushiriki wao katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Majaliwa alitoa pongezi juzi, wakati wa Sherehe za Jubilee ya Kutimiza Miaka 50 ya Total kuhudumu katika soko la Tanzania, ambako alifafanua kuwa, katika kipindi chote cha kuwepo nchini, Total imejipambanua kama moja ya wadau muhimu wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

“Kipekee Serikali ya Awamu ya Tano inaipongeza Kampuni ya Total kwa kuendelea kuwekeza katika kipindi cha miaka 50. Hongereni kwa ubunifu na uwekezaji wenu wa zaidi ya Sh. Mil. 200 kwa ajili ya kusaidia wajasiriamali kupitia mpango ujulikanao kama The African Start Upper Challenge.

“Rai yangu kwa Total ni kuwa, tumieni uwepo wetu nchini kuitangaza vema Tanzania nje ya mipaka. Kadhalika nitoe wito kwa wawekezaji wengine, kuja kwa wingi nchini kuwekeza kama Total, kwa kuwa mazingira ya uwekezaji hapa ni bora na yanaendelea kuboreshwa,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Majaliwa aliitaka Total kufanya uwekezaji mkubwa katika mji wa Dodoma kama ishara ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuhamia huko ambako ni Makao Makuu ya nchi, sambamba na kusapoti harakati za kumaliza changamoto katika Sekta za Afya na Elimu mijini na vijijini.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa, Rais wa Kampuni ya Total Afrika, anayeshughulikia Masuala ya Masoko na Huduma, Stanislas Mittleman, alisema Tanzania ni moja ya mataifa muhimu katika maendeleo ya Total, kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Mittleman alibainisha ya kwamba, kampuni yake iko tayari kwenda na kasi ya mchakato wa Tanzania ya Viwanda unaochakatwa na Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba katika kufanikisha hilo wataendelea kuzalisha, kusambaza na kuuza bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kimataifa.

Alisema Total ni moja kati ya kampuni tano kubwa duniani za uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mafuta, gesi na vilainishi, lakini ikiwa ndio pekee kati ya hizo inayohudumu katika soko la Tanzania kwa miaka 50, tangu ilipoingia nchini mwaka 1969.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, Total itaendelea kutoa huduma bora Tanzania, ambako kuna miradi mingi na mikubwa kama utakavyoona katika video inayoainisha ushiriki wetu katika maendeleo ya taifa na kimsingi tunaahidi tutapanua uwekezaji wetu kulingana na mahitaji,” alisema Mittleman.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Total Tanzania, Tarik Mufaddal, alisema uzoefu walioupata katika kipindi cha miaka 50 ya kutoa huduma nchini, unawapa nguvu na uhakika wa kuendelea kufanya uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bidhaa utakaotoa mchango kubwa kwa uchumi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages