Mpango wa umoja wa Afrika unatafuta wabunifu 60 wa filamu na
televisheni barani kote Afrika kuwa sehemu ya darasa la mwaka 2019.
Vijana 60 kutoka kote barani Afrika – ikiwemo Tanzannia watapata
fursa ya udhamini wa kujifunza uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni
kwa mwaka mzima katika awamu ya pili ya
program ya MultiChoice Talent Factory
Kuanzia tarehe 7 Mei 2019 hadi tarehe 14 Juni 2019, vijana wenye
uchu wa kuwa wabobezi wa filamu watapata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya
usaili utakaotoa wanafunzi 60 watakaodhaminiwa kwa mafunzo hayo ya kitaalamu ya
mwaka mzima yanayoendeshwa katika vituo vitatu barani afrika ikiwemo Nairobi,
Lusaka na Lagos.
Kwa upande wa Tanzania, kuna nafasi nne za udhamini katika awamu
hii ya pili ambapo wanafunzi hao wataungana na wenzao kutoka Kenya, Uganda na
Ethiopia katika kituo cha mafunzo cha Nairobi.
Kwa
wanaotaka kushiriki ni rahisi sana. tembelea
www.multichoicetalentfactory.com kabla ya tarehe 14/06/2019 na kisha fuata
maelekezo ya namna ya kujisajili. Kwa watakaopata tatizo lolote wanaweza kutuma
e-mail info@multichoicetalentfactory.com Au
kupiga simu +255756753201 kwa maelekezo zaidi.
Program ya MultiChoice Talent Factory ilizinduliwa rasmi mnamo Mei
2018, kwa lengo la kuwanoa vijana wa kiafrika katika tasnia ya filamu ili
kuwapa upeo, uwezo, ujuzi na weledi wa kiwango cha kimataifa katika uzalishaji
na biashara ya filamu kwa ujumla.
Cituo hivyo vya mafunzo vinaongozwa na wakufunzi mahiri wenye ujuzi
mkubwa na pia vina vifaa na miundombinu ya Kisasa kuwawezesha wanafunzi
kujifunza uzalishaji filamu wa Kisasa na wa kibiashara.
Kama sehemu ya programu, watengenezaji wa filamu wadogo watapatiwa
mafunzo na uzoefu wa vitendo katika tasnia ya filamu, kwa kuzingatia simulizi
za visa, uzalishaji, sauti na kuongoza na maeneo mengine muhimu. Vituo hivi pia
vinatoa fursa kwa wanafunzi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa
sekta hiyo, kufanya kazi za kuzalisha vipindi vya televisheni, maigizo na kuanda
maudhui asilia ambayo yatakuwa yakirushwa hewani kwa njia mbalimbali ndani ya
M-Net kwa kupitia (DStv)
Darasa la kwanza la programu hii ambalo litakamilika mwezi Oktoba
mwaka huu, tayari limeonyesha mafanikio makubwa ambapo wanafunzi wameshiriki
katika kazi mbalimbali ikiwemo
utengenezaji wa vipindi halisia vya muziki kama Coke Studio, Pambio, Turn-Up na telenovela ya kiswahili
maarufu kama Selina.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso,
amewataka vijana wadogo kuchangamia fursa hiyo adhimu. “Nawasihi vijana wetu wa
Tanzania wenye ari na nia ya kuwa nyota wa uzalishaji wa filamu duniani
kuhakikisha kuwa hawakosi nafasi hii. Wajiandikishe ili waweze kupata fursa
hiii muhimu”
No comments:
Post a Comment