Ofisa Mtendaji Mkuu wa QNET, Malou Calouza (wa kwanza kushoto), na maofisa wa serikali ya Malaysia wakikata utepe kuzindua rasmi kongamano la V-Convetion lililofanyika mjini Penang, Malaysia hivi karibuni. Wengine ni wajumbe wa Bodi wa QNET. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
WAJASIRIAMALI
2,600 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, ni miongoni mwa washiriki 13,000 wa
Kongamano la Kimataifa la siku tano lililoratibiwa na Kampuni maarufu ya
kimataifa ya mauzo ya moja kwa moja, yenye asili ya Asia, QNET.
Kongamano
hilo linalotambulika kama V-Convention, limefanyika Kisiwa cha Penang, nchini
Malaysia likijumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji,
kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na matukio ya burudani.
Kivutio
kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo ilionyesha zaidi ya nembo au lebo 30
za bidhaa za QNET, katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na kampuni
hiyo inayotoa huduma pia nchini Tanzania.
Kongamano
hilo ambalo hufanywa mara mbili kwa mwaka, ni tukio la kipekee ambalo huleta
pamoja wateja na wasambazaji wa QNET kutoka maeneo mbalimbali duniani,
washirika wake wa kibiashara, na pia maofisa wa serikali ili kujionea bidhaa na
huduma za QNET na kuelewa vyema biashara yake.
Ofisa
Mtendaji Mkuu Mteule wa QNET, Malou Caluza, alisema: "Matukio kama haya ya
Kongamano la V-Convention, hutupa fursa ya kuwahudumia wasambazaji wetu na
kuwapa fursa ya kuona na kushuhudia mtindo wa Kuishi Kikamilifu (Absolute
Living) ambao inaongoza biashara yetu.
“Vile
vile V-Convention ni jukwaa bora la kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo
kampuni ya mauzo ya moja kwa moja kama QNET inachochea kwa mamilioni ya watu
duniani kote, kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika jamii," alisisitiza
Caluza.
Bidhaa
mpya zilizozinduliwa mwaka huu ni pamoja na virutubisho vipya kwa ajili ya afya
ya wanaume vinavyoitwa QAlive, huku moja kati ya dondoo zilizoteka hisia za
watu, ikiwa ni sherehe za mahafali ya wateja ambao wamekamilisha kozi zao kwa
njia ya mtandao kupitia qLean.
QNET,
inauza reja reja bidhaa mbalimbali za afya na ustawi, huduma binafsi na urembo,
sikukuu, utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao, ikiwa pia ni miongoni mwa
makampuni 100 makubwa na imara ya MLM
(Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment