Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi ulipowasili mjini Moshi kwa ajili ya mazishi.
Wananchi wakiwa wamejipanga barabarani wakati msafara ukipita.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika leo Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai, Kilimanjaro.
Wananchi wakiwa wamejipanga barabarani wakati msafara ukipita.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika leo Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai, Kilimanjaro.
Waziri
Mkuu anatarajiwa kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali. Ibada ya mazishi
itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni,
Machame.
Mwili
wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu
akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, umewasili Moshi leo ukitokea Dar es
Salaam na kupokekelewa na mamia ya wananchi waliojipanga barabarani.
Jana,
(Jumanne, Mei 6, 2019) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa
Serikali, waliongoza maelfu ya wananchi kutoa heshima za mwisho wakati wa
shughuli za kuaga mwili huo katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hadi mauti yanamfika,
Dkt. Mengi alikuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania (Chairman
of the Media Owners Association of Tanzania - MOAT). Pia aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector
Foundation – TPSF).
Baadhi ya nyandhifa
ambazo Dkt. Mengi aliwahi kushika ni pamoja na Kamishna wa kamati
inayoshughulikia mishahara (Salary Review Commission); Mwenyekiti wa Bodi ya
Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Mazingira Tanzania (NEMC); Mwenyekiti wa vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola
Tanzania (Chairman of the Tanzania Chapter-Commonwealth Press Union-CPU);
Kamishna wa TACAIDS na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – DODOMA.
JUMATANO, MEI 8, 2019.
No comments:
Post a Comment