Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kuichapa Coast Union ya Tanga bao 8-1.
Furaha ya ushindi.
Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kila mmoja akiwa na mpira wake baada ya kufunga mabao matatu yaani ‘hat trick’.
NA MWANDISHI WETU
WAMETISHA! Unaweza kuelezea kwa lugha nyepesi, baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), Simba SC kuibuka na ushindi mnono wa rekodi wa mabao 8-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo umewafanya Simba kuchupa hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ambayo msimu huu walikuwa wanaisikia katika bomba tu kwa zaidi ya miezi 10 waliyokuwa wameikalia mahasimu wao Yanga.
Licha ya ushindi mnono waliovuna, lakini washambuliaji wao wawili, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kila mmoja amefunga mabao matatu yaani ‘hat trick’.
Kwa mabao hayo, sasa Kagere amefikisha mabao 20, katika Ligi Kuu, huku Okwi akifikisha 14 ambayo wanalingana na John Bocco kwenye msimamo wa wafungaji hao.
Mabao mengine ya Simba yamefungwa na Hassan Dilunga na Mzambia Clatous Chama, na kuwafanya Wekundu hao wa Msimbazi watembee mitaani kwa madoido.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 81 kwa mechi 31 na kupaa kileleni mwa msimamo, ikiwaacha Yanga wenye pointi 80 ambayo imeshacheza michezo 34.
Mchezo ulianza kwa kasi kubwa, huku Simba ikitengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo walishindwa kuzitumia katika dakika hizo za mwanzo.
Okwi raia wa Uganda, dakika ya 11 aliwainua mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao la kwanza, akimalizia mpira uliopigwa na kinda Rashidi Juma ambaye alipokea pasi safi kutoka kwa Jonas Mkude.
Coastal Union watajilaumu wenyewe, baada ya Haji Ugando kukosa bao dakika ya 14, kutokana na kupiga shuti kali, lakini kipa Aishi Manula wa Simba kuokoa hatari hiyo.
Mhenga Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 19, baada ya kuunganisha pasi ya Kagere na kuwaacha mabeki wa Costal Union pamoja na kipa, kisha kufunga kirahisi.
Kuingia kwa bao hilo, Coastal Union walizinduka kidogo, na kufanikiwa kupata bao kufutia machozi dakika ya 34 lililofunga na Raizan Hafidh kwa shuti kali alilopiga akiwa nje ya boksi na kuuzamisha mpira wavuni.
Kipindi cha kwanza Coastal, hawakuwa makini kuzuia fowadi za Simba, ambapo walikuwa wanapata nafasi ya kupita hasa katika upande wa kulia wa walinzi wao.
Kipind cha pili kilianza kwa kasi tena, Simba waliendelea kulishambulia lango la Coastal, na dakika ya 49, Okwi alifunga bao la tatu akikamilisha ‘hat trick’ yake baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa na Chama.
Mnyarwanda, Kagere aliifungia Simba bao la nne dakika ya 69, kwa kichwa akiunganisha krosi iliyopigwa na Chama aliyepokea pasi safi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Simba walizidi kulisakama lango la Coastal Union, na walifanikiwa kupata bao la tano kupitia kwa Kagere dakika ya 74, baada ya kumpiga chenga na kumuangusha kipa wa Coastal na kuzamisha mpira wavuni kirahisi akiwa ameitendea haki pasi ya Chama.
Kiungo mzawa Dilunga aliifungia Simba bao la sita dakika ya 81, baada ya kufumua shuti akiwa nje ya boksi akiunganisha krosi ya Mohamed Ibrahim ‘Mo’.
Kagere alikamilisha ‘hat trick’ kwa kufunga bao lake la tatu katika mchezo huo dakika ya 82, na ni bao la saba kwa Simba, baada kuunganisha krosi ya Tshabalala na kumuacha kipa wa Coastal akiushangaa mpira.
Walikiwa hawajui la kufanya, Kiungo Mzambia Chama akahitimisha kisago hicho kwa kufunga bao la nane dakika ya 90, baada ya kupiga shuti la chini lililomshinda kipa wa Coastal, akiunganisha pasi ya Adam Salamba.
Mechi nyingine za Ligi Kuu jana zilimalizika kwa sare, Tanzania Prisons ikitoka suluhu na Ndanda FC, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, huku Mtibwa Sugar ilitoka mabao 2-2 na JKT Tanzania Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Jonas Mkude, Clatous Chama, Said Ndemla/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk78, Rashid Juma/Hassan Dilunga dk68, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi/Adam Salamba dk68.
Coastal Union: Soud Abdallah, Miraji Adam, Ibrahim Ame/ Bakari Mtwiku dk 63, Bakari Mwamnyeto, Adeyum Saleh, Said Jeilan, Haji Ugando, Mtenje Juma, Andrew Simchimcha, Ayoub Lyanga na Raizan Hafidh.

No comments:
Post a Comment