Mshauri Mwelekezi, Nicholas Mbwanji, akitoa mada wakati wa uzinduzi wa Mabaraza ya Ujuzi ya Kisekta uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Taasisi Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF), Salum Shamte, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufungua rasmi Mabaraza ya Ujuzi ya Kisekta.
Washiriki.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba
yake wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Mabaraza ya Ujuzi ya Kisekta
uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake.
Baadhi ya washiriki.
Washirika wa maendeleo wakiwa katika uziduzi huo.
Mwenyenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Sulum Shamte, akimpongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, baada ya kutoa hotuba yake.
Washirika wa maendeleo wakifuatilia mkutano huo.
Mwakilishi wa Sekta ya Kilimo, akitoa neno la shukrani.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako,
akikata utepe sambamba na Mwenyekiti wa Taasisi Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF), Salum Shamte, kuashiria uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa Mabaraza
ya Ujuzi ya Kisekta uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.
Joyce Ndalichako, akipongezwa na Mwenyekiti wa Sekta Binfasi Tanzania
(TPSF), Salum Shamte mara baada kuzinduzi Mabaraza ya Ujuzi ya Kisekta
uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Sekta ya Kilimo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Sekta ya Utalii.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Sekta ya Usafirishaji.
Wadau wa Sekta ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri.
Wawakilishi kutoka Sekta ya Tehama.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri.
Wawakilishi kutoka Tea na Bodi ya Mikopo.
Wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Serilikali kwa kushirikiana na Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wamezindua mabaraza ya ujuzi ya kisekta ili
kujengea uwezo wanavyuo kwenye soko la ajira.
Akizindua mabaraza hayo jijini Dar es
Salaam leo, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stadi, Prof. Joyce Ndalichako
amesema mabaraza hayo yatasaidia kupunguza tatizo la ujuzi katika nyanja
mbalimbali za maendeleo.
“Mabaraza haya yatasimamiawa na kuratibiwa
na TPSF kwa kuwa wao wapo katika nafasi kubwa ya kuzalisha ajira,” alisema
Prof. Ndalichako
Alisema mabaraza hayo yana nafasi nzuri ya
kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuifikisha Tanzania katika uchumi
wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.
“Napenda kutoa ombi kwa sekta binafsi
kuendelea kuwapokea vijana au wanachuo wanaokuja kufanya mafunzo kwa vitendo
(internship) ili kuwajengea uwezo na utayari wa kuingia kwenye soko la ajira,”
alisema
Kwa upande wake, Mwenyeketi wa TPSF, Bwana
Salum Shamte alisema mabaraza yatakuwa ni fursa pekee ya kuunganisha Taasisi
binafsi, Serikali na Wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka nje ya nchi katika
kuleta ufanisi katika maendeleo.
“Tumefikia hatua nzuri mpaka kuyazindua mabaraza haya ambayo
yatakuwa chachu katika kuongeza ujuzi zaidi kwa wahitimu wa vyuo mbambali,”
alisema Bwn. Shamte
Bwana Shamte alisema, TPSF imekuwa ikitoa
ushauri na mapendekezo mbalimbali kwa serikali kupitia Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC) katika ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara na hata Taifa ili yaweze
kufanyiwa kazi.
“Huu ni mwendelezo wa mambo ambayo serikali
imekuwa ikiyafanya kwa kushirkiana na TPSF kwani huko nyuma tumekuwa na
majadiliano mengi yenye tija kwa mustakabali wa ustawi wa uchumi wa Tanzania,”
alisema
Aidha, katika hatua nyingine Bwana Shamte
alisema mabaraza hayo yatajikita katika sekta kuu sita ambazo ni Kilimo,
Utalii, TEHAMA, Uchukuzi, Ujenzi na Nishati, hali ambayo itaongeza
ushirikishwaji mpana kwa wadau katika kukuza
ujuzi nchini.
Kuanzishwa kwa mabaraza hayo kumeungwa mkono
na wadau mbalimbali huku wakieleza ni kwa namna gani yataenda kusaidia katika mnyororo mzima wa kukuza ujuzi nchini.
Bwana Fabian Mwakatuma ambaye ni mjumbe
katika sekta ya kilimo amesema mpango mkakati wa ubia wa Serikali na TPSF
utasaidia sana kupunguza changamoto ya wajuzi katika sekta mbalimbali
“Watu wanaohitimu stashahada na Shahada ni
wengi kwa sasa hapa nchini lakini wengi wao hawana ujuzi na kushindwa kuleta ushindaji katika soko la ajiri, hivyo
uwepo wa mabaraza haya utawaongezea thamani wahitimu wa vyuo mbalimbali,”
alisema Bwana Mwakatuma
Prof. Preksedis Ndomba kwa upande wake
amesema huu ni mpango wa pili wa serikali wa kuhakikisha kunakuwa na viwanda na rasilimali yenye
weledi (ujuzi) katika sekta mbalimbali
“Ujuzi ni ni jambo ambalo ni mtambuka kwani
linagusa maeneo mengi ya kisekta hivyo mabaraza haya yanaenda kuiweka Tanzania
katika ramani nzuri kiuchumi na viwanda,” alisema Prof. Ndomba
Serikali na TPSF wamekuwa na majadiliano ya
mara kwa mara katika kuhakikisha baadhi ya changamoto zilizopo zinapatiwa
ufumbuzi ili kuimarisha mazingira rafiki
kwa upande wa uwekezaji hali ambayo imeleta mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment