Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva, akiwa katika mazoezi ya timu hiyo nchini Misri.
Wachezaji wa Stars wakiwa mazoezini.
Aishi Manula akijifua mazoezini.
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', inaendelea vizuri
na matayarisho yake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Mataifa Afrika
dhidi ya Senegal, Juni 23 mwaka huu katika Uwanja wa 3o June Cairo.
Kutokana na maandalizi yanayoendelea hadi sasa katika
kikosi hicho benchi la ufundi lina imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo
wa ufunguzi na michezo mingine dhidi ya Kenya na Algeria.
Pamoja na wachezaji hao kufanya mazoezi ya uwanjani,pia
wamekuwa wanafundishwa mbinu mbalimbali nje ya uwanja kwa kutumia mikanda
mbalimbali ya video kuwasoma wapinzani wao,kabla ya kuanza kutupa karata yake rasmi
katika mashindano hayo.
Kwa upande wa majeruhi,hadi sasa mchezaji ambaye hatoweza
kushiriki mashindano hayo ni Aggrey Morris,ambaye nafasi yake imechukuliwa na
David Mwantika,ambaye tayari ashawasili ndani ya kambi tayari kwa ajili ya
mashindano.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Emmamuel Amuneke, kimeweka
kambi nchini Misri tangu Juni 7, kwa ajili ya kuweza kupata nafasi ya kufanya
maandalizi ya kina kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment