Spika wa Bunge, Job Ndugai, akizungumza na wachezaji wa Taifa Stars (hawapo pichani) alipowatembelea kambini kwao nchini Misri. Timu hiyo inatupa karata yake ya kwanza ya michuano ya AFCON Juni 23 dhidi ya Senegal.
Picha ya pamoja.
Cairo, Misri
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amekutana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars, katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.
Katika mazungumzo na wachezaji hao, Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21, nchini Misri.
Spika, amewataka wachezaji hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.
Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, alimuahidi Spika kuwa wamepokea salamu za Rais, na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.
Alisema,hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.

No comments:
Post a Comment