HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2019

MASHINDANO YA TAIFA YA RIADHA 2019

MASHINDANO ya Riadha ya Taifa yanatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha Julai 5-6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, mashindano hayo yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Gidabuday, alisema mashindano ya mwaka huu ambayo kikalenda ni makubwa kuliko yote, yanatarajiwa kushirikisha wachezaji 365 na viongozi 31 kutoka mikoa 31.

Alisema katika mashindano hayo michezo 14 inatarajiwa kuchezwa kwa wanaume na wanawake ikiwemo Mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 5,000, 10,000, 4x100, 4x400, Kurusha Mkuki, Kutupa Kisahani, Kutpa Tufe, Kuruka Chini na Miruko Mitatu.

“Tayari mikoa yote imeishapewa taarifa rasmi na yataendeshwa kwa kanuni za Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF), na Shirikisho la Riadha la Tanzania (RT)… Tayari mikoa imetumiwa taarifa ikiambatana na kanuni hizo na idadi ya wachezaji kwa kila mkoa, hivyo tunaiomba mikoa yote ithibitishe rasmi ushiriki wao ili taratibu nyingine za maandalizi ziendelee,” alisema Gidabuday.

Aidha, Katibu huyo aliishukuru Mamlaka la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kwa sapoti yao wanayoendelea kuitoa katika maendeleo ya mchezo wa raidha nchini na kuwaahidi kuzidi kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha utalii katika vivutio vya nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages