HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2019

TRCS yasaidia waathirika kifedha


Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kimezindua huduma ya uahirishaji fedha kwa wakazi 459 wa Kata ya Tandale na Kigogo jijini Dar es Salaam ambao walikubwa na mafuriko miezi miwili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo jana jijini hapa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa TCRC, Mkurugenzi wa Maafa wa TRCS, Renatus Mkaruka alisema, chama hicho kimeamua kuja na huduma hiyo ya kuwasaidia fedha wahanga wa mafuriko.

Mkaruka alisema, mbali na kuwasaidia vifaa mbalimbali wakazi zaidi ya 500 wiki mbili zilizopita lakini hivi sasa wameamua kuja na huduma hiyo ya kuwasaidia kifedha Kaya hizo zilizokubwa na mafuriko ili waweze kuendesha maisha yao.

Alisema kuwa kila Kaya zitapata Sh. 150,000 ambapo kwa sasa wanapokea nusu ya fedha hiyo ambayo ni sh 77,500.

“Hizi Kaya tunazozisaidia ni zile ambazo zimekubwa na mafuriko na ambazo zipo kisheria, sio zile ambazo zimejenga kinyume na sheria,” alisema.

Alisema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku tano mfululizo kuhakikisha wahanga hao wanapata fedha hizo za msaada ili waweze kuendelea kurudi katika hali zao za kawaida.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu alisema, hatua iliyofikiwa na TRCS ni ya kupongezwa kwa kuwa ni njia nzuri ya kuwasaidia waathirika.

Alisema kuwa njia nzuri ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko ni kutoa fedha hivyo ni huduma nzuri iliyofikiwa na Chama hicho.

“Ni matarajio yangu kuwa jambo hili ni zuri na litaigwa na wadau wote kuhakikisha uahirishaji fedha kwa kaya zilizokubwa na maafa zinapata msaada huo na kuweza kurudi katika hali zao za kawaida.

Mkazi wa Kata ya Tandale Mohamed Kibwita aliishukuru TRCS kwa kuwatumbuka kwani msaada huu ni mkubwa na utaleta tija kwetu na kuweza kuinuka kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Pages