HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2019

MOROGORO YA KIJANI YASOMBA UPINZANI 16,470

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika mkutano wa ndani wa kuzindua kampeni ya Morogoro ya Kijani.
 Baadhi ya wanachama walitoka kwenye vyama mbalimbali na kujiunga na CCM katika mkutano huo uliyofanyika jana viwanja vya Jamhuri Morogoro.



NA JANETH JOVIN

UZINDUZI wa  kampeni ya Tuwe Pamoja Tusikubali Kugawanyika na kuifanya Morogoro ya Kijani inawezekana mwaka 2019/2020 katika mkoa huo  imekuwa ya mafanikio baada ya kuwapokea viongozi wa upinzani na wanachama wake takribani 16,470.

Katika Viongozi hao wapo wanachama,  madiwani, wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji pamoja na viongozi wa ngazi mbali mbali waliotoka katika vyama vya upinzani na kujiunga na CCM.

Wanachama hao waliojiunga na Chama hicho ni kutoka  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao ni 12,547,Chama cha ACT-Wazalendo 508
,Chama cha Wananchi CUF, 3217 huku Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakiwa 18.

Akiwapokea Wanachama hao huku akizindua Kampeni hiyo,
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CCM Bara Rodrick Mpogolo anasema uzinduzi wakampeni hiyo ni muendelezo wa kuwafanya wanaccm wanakuwa na umoja pamoja na ushirikiano.

Anasema mara nyingi wamekuwa wakishindwa katika baadhi ya chaguzi kutokana na kutokuwepo kwa umoja na mshikamano baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho.

"Mara nyingi tumekuwa tukishindwa katika Chaguzi mbalimbali kutokana na kuwepo Kwa migogoro ndani ya Chama hivyo basi naamini tukiwa na umoja na mshikamano kupitia Kampeni hii tutashinda katika Chaguzi zinazokuja za serikali za mitaa na vitongoji," anasema

Mpongolo anasema ili chama hicho kiendelee kushika dola ni muhimu kwa wanaccm kuacha tabia za chuki, malumbano, Fitina na kupakana matope kwani wao ni familia moja.

Aidha anasema katika kuelekea Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020,viongozi wa mkoa Wa Chama wanatakiwa kuhakikisha nafasi za uongozi zinajazwa ili kuwa na Jeshi imara litakaloweza kuwapatia CCM ushindi.

"Kila mwanachama wa CCM anatakiwa afahamu kuwa yeye ndio anawajibu Wa kuhakikisha CCM inashinda Kwa kuongeza wanachama wapya kwani nguvu ya wanachama ni wanachama wenyewe," anasema Mpogolo

Aidha Mpogolo anasema ni muhimu Kwa viongozi hasa wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanatenga muda wa kusikiliza kero na shida za wananchi.

"Kila kiongozi anapaswa kupanga muda wake wakusikiliza wananchi na kuwasaidia kuzitatua kwani wananchi ndio wapiga kura wetu na wametuweka katika kuwatumikia," anasema

Kwa Upande wake Mkuu Wa Mkoa Wa Morogoro Dk.Steven Kabwe anasema katika kipindi cha mwaka mmoja viwanda vidogo na vya kati
186 vimejengwa katika mkoa huo.

Kabwe anasema kuhusu Kilimo Mkoa wa Morogoro unaendelea vizuri katika sekta hiyo ambapo miaka ya nyuma asilimia 32 ndio walikuwa wanalima lakini Kwa mwaka huu takribani asilimia 43 ya watu wa Morogoro wanafanya kilimo.

Pia anasema Kwa Mwaka jana walipata ziada ya Chakula takribani milioni 1.7 hali hiyo inadhihirisha kuongezeka Kwa shughuli za kilimo katika mkoa huo.

"Katika Upande Wa Wafugaji kila mwaka wafugaji 6000 upewa elimu ya mafunzo juu ya namna bora ya kuboresha na kufanya ufugajinwa kisasa," anasema Kabwe na kuongeza

"Hali ya usalama Kwa mkoa umetulia Kwa asilimia 90 kulingana na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na mapigano ya wakulima na wafugaji kupigania Ardhi ambapo imepelekea Mkoa wa morogoro kuwa na Kanda màalum ya Ardhi," anasema

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocenti Kalogelesi ,anasema ni muhimu kujipanga ili washinde katika uchaguzi wa serikali za mitaa ,wabunge na Urais 2020.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka anasema kampeni hiyo ya Tuwe pamoja tusikubali kugawangika  inamalengo makubwa na dhamira moja ya kuonyesha mshkamano wao na kuangalia ni kwa namna gani wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Anasema kupitia programu hiyo wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha Morogoro inashika majimbo yote hata yaliyochukuliwa na wapinzani.

"Naibu Katibu Mkuu Mpogolo tupelekee salamu zetu Kwa Mwenyekiti wetu kuwa Morogoro tumejiandaa vizuri na programu hii na tunahakikisha tunafanya kazi vizuri na dhamira yetu ni kuonyesha mshikamano na kuhakikisha tunashinda katika Chaguzi zote," anasema Shaka.

No comments:

Post a Comment

Pages