Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdullah Ulega akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Watumishi wa Taasisi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wanaopata mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwakilishi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa Japan Kentaro Akutsu akitoa namna wanavyotoa ufadhili wa Mafunzo kwa Watumishi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia ikiwa ni njia kuongeza ajira kwa vijana katika nchi hiyo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo yanayoendeshwa na Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Watumishi wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wakiwa katika mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchni (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Yahya Mgawe akitoa taarifa namna wanavyotoa mafunzo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Watumishi wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini Somalia yanayofanyika katika cha Uvuvi Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema katika kufikia uchumi wakati sekta ya Uvuvi ni sekta ambayo inahitaji wawekezaji makini ikiwemo kutumia wataalam wa Uvuvi wanaosoma vyuo vya ndani.
Hayo ameyasema Ulega wakati akifungua mafunzo ya Watumishi 20 wa Taasisi za Sekta ya Uvuvi nchini walioletwa na Shirika la Kimataifa la Japani (JICA) katika Wakala ya vyuo Uvuvi (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Amesema sekta ya Uvuvi imekuwa na michango mingi Bungeni katika kuona nchi inanufaika katika kuleta maendeleo kwa kufikisha dhamaira ya serikali ya kufukia uchumi wa Kati.
Ulega amesema kuwa kutokana na Wakala ya Vyuo vya Uvuvi kufanya vizuri ndio maana nchi nyingine wanakuja kujifunza nchini Tanznaia.
Amewasaa wasomali wanaopata mafunzo wakayatumie katika kuwapa maendeleo nchini mwao.
Amesema kuwa Wakala ya Vyuo vya Uvuvi kwa miaka miwili Zaidi ya wageni 770 wamepata mafunzo katika Wakala hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo Vya Uvuvi nchini (FETA) Yahaya Ibrahim Mgawe amesema kwa miaka hivi karibuni wameisha to mafunzo kwa wanafunzi Mia Saba sabini kutoka nchi mbalimbali moja ya mafunzo nibutawala Uvuvi menejimenti na masoko.
No comments:
Post a Comment