Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza jambo na Viongozi
wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na
Utalii cha nchini China kijulikanacho
kwa jina la JXCFFS mara baada ya kuwatambulisha wageni hao Bungeni Dodoma leo
waliokuja nchini kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa mafunzo
watumishi na wadau wa utalii nchini. (Picha na Wizara
ya Maliasili na Utalii).
Dodoma, Tanzania
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii, suala la kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.
Imesema nguvu nyingi
kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo
ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha
ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.
Hayo
yamesemwa
leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni
na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS.
Amesema lengo mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya
China na Tanzania
katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.
Mkutano huo umehudhuriwa na ujumbe kutoka China
ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa
Wizara Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.
Amesema ni muhimu kwa
watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza
lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna
uwezekano kwa Watanzania kujifunza.
Naye Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali
likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo
Watumishi hao
Ameongeza kuwa tayari
wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.
Kwa upande wake,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa
Chuo hicho ili kujengeana uwezo baina ya Serikali ya Tanzania na China.
No comments:
Post a Comment