Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizindua mkataba wa huduma bora kwa mteja wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi, Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.
Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla, akizindua amzezindua
Mfumo wa uendeshaji wa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015 Quality management
system) wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau
mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru
jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA, Dk. Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa, Kamishna Nsato Marijani na
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa utalii wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, ni miongon mwa waalikwa walioshiriki hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii.
Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dk. Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC), Dk. Ayoub Ryoba, akiwa na Mkurugenzi wa Channel Ten, Jafary Aniu, pia walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika hafla hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Mawasiliano TANAPA, Pascal Shelutete, akitangaza utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wadau wa utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akiwa katika pich ya pamija na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ,Emilian Mallya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa tatu katika kutangaza hifadhi za taifa .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji, Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Ryoba (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mshindi wa jumla ,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Adventure pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi, Mjumbe wa Bodi -TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jeryy Muro.
Washindi wa tuzo za Gold wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Na Dixon Busagaga
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa mara ya kwanza limekabidhi tuzo kwa Wadau
mbalimbali wa masuala ya Utalii na
Uhifadhi ,tuzo zilizokabidhiwa na Waziri wa Malisili na Utalii jijini Arusha kwa
lengo la kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika masuala ya Utalii na
Uhifadhi.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya
Maount Meru, Waziri Dk. Kigwangalla pia amezindua Mfumo wa uendeshaji wa
viwango vya kimataifa yaani ISO 9001:2015
Quality management system pamoja na mkataba wa huduma bora kwa mteja.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi kutoka kampuni na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na
masuala ya Utalii na Uhifadhi ,Mgeni rasmi ,Waziri ,Dkt Hamisi Kigwangala
aliipongeza TANAPA kwa uamuzi wa
kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.
“Niwapongezeni
TANAPA ,Bodi ya wadhamini na Menejenti ya TANAPA mnafanya kazi nzuri sana hasa
katika kuisimamia ipasavyo sekta ya utalii, Hongereni sana.”alitoa pongezi hizo
Dkt Kigwangalla.
“Nampongeza
sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka mkazo kwenye sekta ya miundombinu
na sekta ya anga kwani zimekuwa kichocheo katika ukuaji wa sekta ya utalii,niwahakikishie
wadau wa Sekta binafsi katika sekta hii ya utalii, tutaendelea kuwapa
ushirikiano wa kutosha lengo ni kuhakikisha tunakuza na kuendeleza sekta hii
kwa kasi kubwa kabisa.”aliongeza Dkt Kigwangalla.
Dkt
Kigwangalla alisema tuzo walizopata wadau wa sekta ya Utalii kwa kazi nzuri
wanazoendelea kufanya ziwe chachu katika kuimarisha ushindani katika utoaji
huduma bora katika sekta ya utalii ambapo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi
yetu.
“Natoa
wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuwekeza katika maeneo ya usafiri na malazi
kwenye maeneo ya Kusini na Magharibi mwa nchi yetu.”alisema Dkt
Kigwangalla.
Mjumbe
wa Bodi ya TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani aliyemwakilisha mwenyekiti wa bodi
hiyo,Jenerali George Waitara alisema uzinduzi wa Mkabata wa
Huduma kwa Mteja utawezesha utoaji huduma kwa Haraka, ufanisi na kwa wakati ili
kuondoa malalamiko na urasimu usio na tija kwa pande zote mbili.
“Sisi
kama Bodi tunaahidi kuendelea kusimamia sekta hii kwa kikamilifu ili iwe na
mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.”alisema Kamishna Nsato.
Kwa
upande wake KAmishna Mkuu wa Uhifadhi ,Dkt Allan Kijazi alisema TANAPA
inatambua mchango mkubwa wa wadau wetu wote katika sekta ya utalii kwa jitihada
zote wanazozifanya katika sekta hiyo ikiwemo kuiletea heshima nchi.
“
Tunathamini na tutaendelea kuthamini kila mdau anayefanya kazi na TANAPA,shirika
limefanikiwa kuongeza ulinzi wa rasilimali zetu, tutaendelea kuimarisha
miundombinu ili kuwezesha kufikika kwa urahisi katika hifadhi zetu.”alisema Dkt
Kijazi .
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii nchini (TATO) Wilbert
Chambulo ameishukuru TANAPA kwa tuzo hizo na kwmba shirika hilo limekuwa
likijitoa kwa wadau wa utalii hali ambayo imechangia kampuni hizo kukua
kiuchumi.
“TANAPA
imebadilika sana.nakuahidi Mhe. Waziri Tutaendelea kulinda na kudhitibi
uharibufu wa hifadhi zetu na nina kukabidhi magari mawili kwa ajili ya zoezi
hilo”alisema Chambulo.
No comments:
Post a Comment