HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

WADAU WA MASUALA YA FEDHA KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA WA MWAKA 2019

Kamati ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9), imepanga kufanya mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau wote wa masuala ya fedha (Public Hearing) kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019).
   
Mkutano huo wa kusikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) unatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 20 na Ijumaa tarehe 21, 2019 kuanzia saa Nne Asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao kabla Muswada huo haujapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA.

No comments:

Post a Comment

Pages