HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2019

Aiomba Serikali kuweka sheria kali kwa wanaokopi kazi za wabunifu

Na Janeth Jovin

MBUNIFU wa mavazi ya stala na vilemba, Said Ndee, ameiomba Serikali kuweka sheria kali kwa wale wote wanaiba na kukopi kazi za wenzao waluzozibuni.

Ndee ametoa maombi hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara kuhusiana na mavazi pamoja na vilemba anavyovibuni.

Anasema wao wabunifu wadogo wamekuwa wakibuni mavazi mbalimbali lakini wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya watu kukopi kazi zao na kuzifanya za kwao.

"Sasa hivi kuna dimbwi kubwa la watu kukopi kazi za watu ambao wanatumia muda mwingi kuzibuni hivyo basi tunaiomba serikali iweke sheria kali kwa watu hawa ili wasiweze kufanya jambo hilo ambalo linakwamisha kuendelea kwa wabunifu hawa, " anasema.

Hata hivyo Ndee amewataka watanzania kuvipenda vitu vya hapa nyumbani kwa kununua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuwainua wajasiriamali.

"Ni muhimu kwa watanzania kununua bidhaa za kitanzania na wakija sabasaba katika banda la walemavu wataikupa Pichichi Turbans Fashion Designer tutawauzia mavazi ya stala na viremba kwa bei nafuu kabisa, " anasema

Hata hivyo anasema uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwa nywele bandia na rasta zinazoingizwa nchini utaweza kuwabadirisha wanawake kutoka kutumia nywele hizo na kuanza kuvaa viremba.

No comments:

Post a Comment

Pages