Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019. (Picha zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Sehemu ya washiriki wakifatilia kwa karibu hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Bi Gloria Emmanuel ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Monduli wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Shaban Minja ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Same wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Jitihada za kuongeza uzalishaji zinakuwa na mafanikio hafifu kutokana na
kutotumia teknolojia sahihi zinazoendana na mahitaji na wakati; Mathalani,
matumizi ya zana za kulimia ama zikiwa za mkono au zinazokokotwa na wanyamakazi
au matrekta, zimekuwa zikisababisha mmomonyoko wa udongo hasa katika maeneo
yasiyo tambarare na kusababisha upotevu mkubwa wa rutuba na kujengeka kwa jasi
(hard pan).
Kwenye maeneo yenye mvua chache njia hizo za kilimo cha kukatua ardhi hazitunzi
unyevu na kusababisha uzalishaji kuwa wa chini hasa pale panapokuwa na vipindi
virefu vya ukame (dry spells) kama ilivyotokea msimu huu wa kilimo
katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe
03 julai 2019 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya
kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi
nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa,
Jijini Dodoma.
Mhe Hasunga anasema kuwa kwa sababu hiyo basi, ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kubadilisha mifumo inayotumiwa katika kuandaa
mashamba ili kupata matokeo mazuri.
Amewashukuru Washirika wa Maendeleo (Development Partners)
pamoja na Wadau wote wa Kilimo Hifadhi waliowezesha kufanikisha warsha hiyo
muhimu wakiwemo African Conservation Tillage Network (ACTN), Canadian Food
GrainBank (CFGB), Diocese of Central Tanganyika (DCT), na Conservation Farming
Unit (CFU) –Tanzania.
Alisema juhudi hizo wanazofanya za kuendeleza Kilimo Hifadhi kwa
kushirikiana na Serikali kwa maendeleo ya wakulima na Taifa kwa ujumla, ni
sehemu ya mwelekeo wa kufikia Uchumi wa Viwanda kwa kukuza uzalishaji wenye
tija.
Aliongeza kuwa jitihada hizo zinaendana na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013
na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural
Sector Development Programme - ASDP II) ambazo zinahimiza
usimamizi endelevu wa matumizi bora ya maji na ardhi, kuongeza tija na faida
katika uzalishaji, biashara na kuongeza thamani ya mazao na kuiwezesha Sekta
katika uratibu, ufuatiliaji na tathmini.
Kadhalika Waziri Hasunga amesema kuwa
ili kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo, Serikali imeongeza juhudi za
kuwaunganisha wakulima na masoko, huduma za kifedha, usindikaji wa mazao na
kuongeza thamani.
Alisema kuwa katika kutimiza azma hiyo,
Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Kilimo inaendelea Kuweka mazingira mazuri
yanayovutia uzalishaji na uwekezaji, Kuimarisha mafunzo, Utafiti, ubunifu na
uenezaji wa teknolojia za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na
Kilimo Hifadhi na kuboresha Huduma za Ugani, Kuongeza uzalishaji na tija katika
kilimo, uongezaji thamani ya mazao, kuimarisha ushirika, kuwaunganisha wakulima
na masoko na huduma za fedha; na Kuhamasisha na kusimamia matumizi ya
teknolojia za kisasa za kilimo ikiwemo teknolojia za kilimo hifadhi kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya
kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa (Mb) alisema kuwa
serikali inapaswa kujipanga vizuri kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini kwa
kufanya utafiti wa kina kwa utafiti ndio nguzo ya kilimo.
Alisema kuwa
asilimia kubwa ya mbegu zinaagizwa nje ya nchi hivyo aliiomba aserikali
kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo hususani katika kuendeleza sekta ya mbegu.
Amesema
Tanzania bado kuna tatizo kubwa la Masoko kwani wakulima wengi wanazalisha
mazao yao lakini hawana mahali pakuyauza kwa bei nzuri huku wengine wakishindwa
kusafirisha mzao yao kutokana na miundombinu kutoimarika kwa kiasi kikubwa.
Kadhalika ameipongeza wizara ya Kilimo kwa kuanzisha mchakato wa mapitio ya
sera ya kilimo ya 56mwaka 2013 itakayopelekea kuwa na sheria mpya ya Kilimo.
Awali akitoa salamu za wizara ya Kilimo kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe alisema kuwa Lengo la warsha
hiyo ni kuwawezesha washiriki kupata uzoefu na kufahamu juhudi na matokeo ya
kazi za kuendeleza kilimo hifadhi zinazofanyika nchini na kuweka mpango
utakounganisha, kuratibu na kusimamia shughuli za kuendeleza matumizi bora na
endelevu za teknolojia za kilimo hifadhi nchini.
Alisema kuwa matumizi ya
kilimo cha kisasa (smart agriculture) ikiwa ni pamoja na
kilimo hifadhi ni nguzo katika kuendeleza kilimo nchini kwa kongeza tija,
kuboresha ardhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa katika maeneo
yanayopata mvua chache.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Katika
miaka ya hivi karibuni, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi
mwaka. Tathmini zilizofanywa na Wizara zinaonyesha kuwa
karibu hekta 40,000 nchini zinalimwa kwa kutumia kilimo hifadhi na
matokeo yanaonyesha kuwa mavuno (yields) wanayopata wakulima
kutoka kwenye mashamba ya kilimo hifadhi ni mazuri hata wakati wa mvua chache.
Aliongeza kuwa Katika kipindi
hiki, ambacho Serikali inajitahidi kuongeza miundo mbinu ya umwagiliaji na
kuongeza matumizi ya mbolea za viwandani kwa gharama kubwa ili kuongeza tija na
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, matumizi ya teknolojia ya
kilimo hifadhi ni njia mbadala ya kufikia malengo hayo kwa haraka na kwa
gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment