Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna Benki ya NMB
ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Barabara ya Pugu, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Msimamizi wa
Banda la NMB ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud.
Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya Viwanja
vya Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari kuelezea namna Benki ya NMB ilivyojipanga kukidhi mahitaji ya
wateja wao ndani ya Maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara
yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Pugu,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa NMB, Badru Idd akiwa
katika mkutano huo.
Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB (kushoto) akipata huduma ndani ya Banda la Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya
NMB imejipanga kutoa huduma zote za kibenki wa washiriki na wananchi
wanaotembelea maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea
viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Pugu jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na wanahabari leo ndani ya Banda la Benki ya NMB, Meneja wa Kanda wa
NMB, Badru Idd alisema benki hiyo imejipanga kutoa huduma zote muhimu za
kibenki ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yote kwa washiriki wa
maonesho hayo.
Aliwataka
washiriki na wananchi wengine kutoumiza vichwa pindi watakapo hitaji
huduma za kibendi ndani ya viwanja hivyo kwani benki hiyo imejipanga
kutoa huduma zote muhimu za kibenki.
Aidha
aliwaomba wananchi kutembelea Banda la NMB kujipatia huduma mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya huduma mpya na bora kwa wateja
wake.
Kwa
upande wake Meneja Msimamizi wa Banda la NMB ndani ya viwanja vya
Sabasaba, Bi. Kidawa Masoud aliongeza kuwa huduma za NMB ndani ya
maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa ni sawa na huduma zinazotolewa na
tawi lolote kubwa la NMB hivyo kuwashauri wananchi kutembelea kipata
huduma zote muhimu ndani ya viwanja hivyo.
"...Huduma
za NMB zinazotolewa katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara
yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere ni sawa na huduma
zinazotolewa na tawi letu lolote...tuna mambo mengi mazuri kwa wateja na
watakaotutembelea waje kwa wingi wafurahiye huduma zetu," alisema Bi.
Masoud.
No comments:
Post a Comment