Waziri wa Viwanda na Biashara,
Innocent Bashungwa, akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Na Tatu Mohamed
MAKAMU
wa Rais, Samia Hassan Suluhu anatarajia kufungua rasmi kesho maonyesho
ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yaliyoanza Juni 28
mwaka huu na yanatarajia kumalizika Julai 13, mwaka huu.
Maonyesho
hayo ambayo ni ya siku 10 huvuta zaidi ya watu 350,000 na ni moja ya
fursa bora ya kupanua biashara ambayo hutoa nafasi ya kuwasiliana moja
kwa moja na wateja waliopo na wapya, pia ni jukwaa la kulinganisha
bidhaa na huduma zinazohusiana zenye ushindani.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Julai 1, 2019 jijini Dar es Salaam viwanja
vya katika maonesho hayo, yenye kauli mbiu ya 'Usindikaji wa Mazao ya
Kilimo kwa Maendeleo ya Viwanda', Waziri wa Viwanda na Biashara,
Innocent Bashungwa amesema maonesho ya mwaka huu yatakuwa tofauti na
miaka ya nyuma.
"Tofauti ni kwamba sabasaba ya mwaka huu
tunataka iwe jukwaa la kujipambanua katika uchumi funganishi wa
viwanda. Sabasaba ndo tunataka iwe fursa ya kuwakutanisha watu
mbalimbali," amesema.
Ameongezea kuwa katika siku
yenyewe ya sabasaba ambayo huadhimishwa Julai 7, kila mwaka kutakuwa ni
siku maalumu ya mazao ya kimkakati.
Amebainisha kuwa kwasasa jumla ya nchi 35 zimeshiriki maonesho haya, huku taasisi na kampuni za ndani zikiwa 3250.
No comments:
Post a Comment