Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja
wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, akimsikiliza
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya (kulia) wakati
akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO
S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba
Saba jijini Dar es Salaam leo.
Na Tatu Mohamed
KAMPUNI
ya simu ya mkononi ya Tigo Kwa kushirikiana na Kampuni ya Tecno
imezindua simu mbili aina ya Tecno 3G na 4G Kwa lengo la kuwafikia
watanzania wengi hususani wa kipato cha chini.
Akizungumza
leo Julai 1,2019 katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya
maonyesho ya 43 ya kibiashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba, Meneja
wa Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, Mkumbo Myonga amesema uzinduzi wa
simu hizo unadhihirisha mkakati wa kampuni ya tigo kuendelea kufanya
ubunifu wa kidigitali nchini.
Amesema simu hizo zitaweza kuwapa fursa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa simu, watumiaji wa huduma za data na intaneti.
"Tunayofuraha
kushirikiana na Tecno kuzindua aina mbili za simu za kisasa kwa mwaka
huu 2019 ambazo ni simu aina ya Tecno S3 na R7, kwa sasa zinapatikana
kwa kampuni hiyo ya tigo tu," amesema na kuongeza
"Simu hizi zinaofa ya mwaka mmoja wa bure wa kutumia intaneti Kwa wateja watakaozinunua na bei yake in ndogo kwa wanunuaji,".
Naye
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tecno, Eric Mkomoya amesema kuzinduliwa
kwa simu hizo kumelenga kuwawezesha wananchi kutumia simu za kisasa
zenye teknolojia mpya.
Amesema
simu ya Tecno R7 imetengenezwa ikiwa na kioo cha ukubwa wa inchi 5,
kamera yenye uwezo wa mega 5 huku Tecno S3 ikiwa na kioo cha mbele inchi
4.
No comments:
Post a Comment