Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
SERIKALI
imesema bado bidhaa za viungo na zile zitokanazo na zao la mwani
zinazozalishwa nchini hazina ubora stahiki jambo linalosababisha
wazalishaji kushindwa kuzipeleka katika masoko mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
Pia imesema
mdalasini wa Tanzania unahitajika sana duniani, kutokana na kutokuwa
na kiwango cha kemikali na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Kadhalika zao la Iliki linahitajika kwa wingi Pakstani ambapo soko lake kubwa Kimataifa.
Waziri
wa Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibari, Balozi Amina Salum
Ali amesema hayo katika siku maalum ya bidhaa za viungo na
mwani katika maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Amesema
kilimo cha mazao ya viungo kina tija na kimekuwa kuwalipa sana na
kuhimiza wazalishaji kutumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa zenye
ubora.
"Ni vyema
wazalishaji kutumia teknolojia ya kisasa, pia vyombo vya taifa
kuangalia teknolojia rahisi ya kutumia yenye kuwasaidia wananchi.
"Pia
nahimiza kuwepo kwa ubunifu katika kutengeneza bidhaa zinazotakiwa na
hata kuwa na vifungashio imara na bora ili kumudu soko la ndani na
nje ya nchi," amesema.
Awali
akizungumza katika siku hiyo, Mkurugenzi wa Tantrade, Edwin Rutageruka
amesema zipo fursa mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa za viungo na
kuwataka wazalishaji kushirikiana na Mamlaka hiyo ili kuweza kufika
mbali.
Amesema wapo
baadhi ya wafanyabiashara ambao sio wakweli wakiahidi kusambaza
bidhaa katika masoko ya kimataifa lakini wakiwa hawawezi kufanya
hivyo.
No comments:
Post a Comment