HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2019

VETA YAJA NA MFUMO WA KUPUNGUZA FOLENI

Mfumo wa kumsaidia trafiki unavyoweza kufanya kazi.
 Mwanafunzi kutoka Chuo cha Veta Chang'ombe, Innocent Swanga akionyesha jinsi mfumo wa kumsaidia trafiki unavyoweza kufanya kazi.

Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imebuni mfumo  maalumu kwa ajili ya kumsaidia trafiki kuongoza magari bila ya kusimama katikati ya barabara.

Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yalioanza Juni 28, mwaka huu Mwanafunzi na Mwanagenzi wa umeme kutoka Veta Changombe , Innocent Swanga amesema lengo la mfumo huo ni kumsaidia trafiki kuepuka kero mbalimbali asimamapo barabarani ikiwemo kugongwa na magari.

Amesema wazo la kutengeneza mfumo huo liliwajia kutokana na kuona kero iliyokuwepo katika barabara na kuona matrafiki wamekuwa wakipata shida na kuatarisha maisha yao pindi wanapokuwa barabarani.

Amesema mfumo utamsaidia trafiki kufanya kazi bila ya kutumia nguvu wala kusimama katikati ya barabara hivyo kumpa urahisi zaidi wa kuangalia ni sehemu gani ambapo pamezidiwa na foleni na kuponyeza mfumo huo kisha taa zitawaka.

"Teknolojia hii bado haijaanza kufanya kazi tumepeleka wazo katika Ofisi husika ili waweze kuungalia kama unaweza kusaidia kupunguza adha ya foleni," amesema Swanga.

Ameongeza kuwa mfumo huo utafungwa pembeni ya barabara na kuunganishwa katika taa za barabarani  ambapo trafiki atakuwa akibadilisha ni sehemu gani ambapo magari yameonekana kukaa kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Pages