SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC )limewataka wananchi kutembelea banda lao lililopo katika viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya 43 ya Biashara maarufu sabasaba kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali kuhusu meli na usafiri wa majini.
Akizungumza katika maonyesho hayo Kaimu Mkurugenzi wa TASAC Mhandisi Japhet Loisimaye anasema pamoja na uchanga wa shirika hilo lakini yapo mambo mbalimbali ambayo wanayatekeleza kwa majukumu wa sheria.
Anasema kwa mujibu wa sheria namba 21 ya mwaka 2003 shirika hilo linajukumu la kudhibiti Usalama wa vyombo vya majini hivyo hakuna chombo ambacho kitaruhusiwa kuingia majini bila kutambulika ubora wake na anayekiuka hilo amekiuka sheria.
Loisimaye anasema utekelezaji wa sheria hiyo ni kutokana na Tanzania kuwa mwachama wa Shirika la Meli Duniani (IMO) ambalo linaitaka kila nchi mwananchama kusimamia usalama wa vyombo vya majini.
"Unapokuwa mwanachama wa IMO lazima usimamie usalama wa majini kwa mujibu wa kanuni zao na TASAC kwa niaba ya serikali ndiyo inayosimamia usalama wa vyombo vya majini hapa nchini hivyo ni lazima tufanye kazi zetu kwa kufuata sheria, " anasema.
Hata hivyo Mhandisi Loisimaye anasema tayari kanuni 22 zimekwisha kutengenezwa ili kusimamia sheria ya usafiri wa majini ya mwaka 2003 namba 21 na ya TASAC 2017 inatengenezewa vitendea kazi.
"Kanuni ndio inayokwenda kumwelekeza mwenye meli afanyaje hasa ikianiasha majukumu ya mdhibiti na mwenye meli ,kwa shughuli zote za usafirishaji wa majini sisi ndio tunashughulika nayo"anasema.
Aidha anasema ni fursa sasa kwa watanzania kujitokeza kujifunza namna shirika hilo linavyofanya kazi kuhakikisha usalama wa vyombo vya majini vinakuwa katika usalama.
No comments:
Post a Comment