Na Janeth Jovin
SERIKALI imesema kuwa imeanzisha vyama vya wanawake wafanyabishara mipakani ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa ana kwa ana wa wafanyabishara wa sekta ya matunda na mbogamboga, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Edwin Rutageruka (pichani), anasema mpaka sasa wanawake 300 wameanza kunufaika kupitia vyama hivyo ambapo kila mpaka watahakikisha wanajenga ofisi ya vyama.
Anasema ofisi hizo ziianzishwa zitaratibu shughuli za kibiashara na kupatiwa vibali vya kufanya biashara ndani na nje ya mipaka.
Rutageruka anasema wafanyabishara hao watarasimishwa kwa Wale ambao wasio rasmi.
"Kupitia vyama hivyo vitaandaa masoko maalum kwa ajili ya kufanya biashara wenyewe na kuhakikisha wanapata masoko makubwa yatakayowanufaisha, " anasema.
Anasema wameamua kufanya hivyo baada ya kugundua asilimia 70 ya wafanyabishara wanaofanya shughuli zao mipakani ni wanawake.
"Vyama hivi vya wanawake pia vitawasaidia kuwapa fursa katika biashara zao na kuwafanya waje kuwa wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa zao, " anasema.

No comments:
Post a Comment