Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Mobisol akizungumza na wateja waliofika katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba'.
Na Janeth Jovin
IMEELEZWA kuwa Tanzania kwa sasa ni nchi yenye fursa kubwa ya kuzalisha umeme unaotokana na nishati ya jua ambao unatoa fursa kwa watu wengi hasa wahishio vijijini kupata umeme unaotumia nishati hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam leo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Mkuu wa Kitengo cha Masoko Kampuni ya usambazaji wa huduma za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua (Mobisol), Francis Shenyagwa, amesema ni muda muafaka kwa watanzania kuanza kuwa na mtazamo chanya kuhusiana na manufaa ya muda mrefu yanayotokana na matumizi ya nishati ya jua.
Anasema umeme wa jua ni chanzo kinachofaa cha nishati mbadala majumbani na nchi nyingi tayari zimegundua ukweli na zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya
umeme vilivyozoeleka kama makaa ya mawe.
"kwa kutambua umuhimu wa nishati ya umeme unaotokana na jua Mobisol tumeingiza sokoni mifumo inayokwenda mbali zaidi ya ile ya kukidhi haja ya upatikanaji wa mwanga majumbani tumekuja na vifaa ambavyo vinakidhi haja nyingi ambapo bidhaa zetu ni bora ikilinganishwa na vile vinavyotumiwa majumbani kwenye maeneo ambayo hayana umeme, kama mshumaa na taa za chemli," anasema
Shenyagwa anasema wapo nchini kwa zaidi ya miaka minne sasa hivyo wanahakikisha huduma wanayotoa inakidhi mahitaji ya watanzania na kuwafikia watu wanaoishi katika maeneo ya ndani hususani mashambani yasiyofikika kwa urahisi .
"Sisi ni wadau wa maendeleo wa kudumu nchini, kwenye jitihada za kufikisha huduma za umeme unaotokana na nguvu ya jua kwa maeneo yasiyokuwa na umeme, tupo tayari kuwekeza zaidi katika kupanu wigo wa huduma zetu dhamira yetu ya kusambaza umeme wa jua katika kila sehemu nchini inajidhihirisha wazi kwa jinsi ambavyo tumejikita shughuli zetu hadi maeneo mengi ya mashambani, ambapo kipato ni cha msimu na kufanya malipo kutoka kwa wateja yawe ni ya kusuasua," anasema Shenyagwa.
Aidha anasema bado kuna mambo ya ziada yanayostahili kufanywa ili kujenga usimamizi dhabiti wa soko la bidhaa zinazotumia umeme wa jua ili kuhakikisha kuwa wateja
wanapata bidhaa bora.
No comments:
Post a Comment