Wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya ziara ya kujifunza Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).
Mionzikutembelea Arusha, 09 Julai, 2019
Wanafunzi 32 wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili (MUHAS) Jumatatu tarehe 08 Julai, 2019 walifanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) yaliyopo Njiro, Jijini Arusha.
Lengo la ziara hiyo ya siku moja (1) lilikuwa ni kujifunza
matumizi mbalimbali ya teknolojia ya nyuklia yanayofanyika hapa nchini pamoja
na udhibiti wake.
Bw. Didas Shao ambaye ni Mtafiti wa masuala ya mionzi sehemu za kazi, amesema
kuwa wanafunzi hao wameweza kujifunza juu ya matumizi mbalimbali
ya teknolojia ya Nyuklia inavyotumika hapa nchini katika sekta
za viwanda, kilimo, mifugo, ujenzi, maji, migodi pamoja matumizi ya teknolojia
hiyo katika sekta ya afya, sanjari na
udhibiti wake ili kutokuleta madhara kwa wagonjwa, wananchi pamoja na mazingira.
Wanafunzi hao pia waliweza
kujifunza namna ya kukabiliana na majanga yanaohusiana na teknolojia ya nyuklia na kuweza kujua sheria mbali mbali
zinazosimamia teknolojia hiyo hapa nchini.
TAEC inaendelea kuwakaribisha wadau mbalimbali, wananchi na
wanafunzi katika ngazi zote za elimu hapa nchini kuanzia shule za msingi, sekondari
na vyuo vya elimu ya juu ili kufika katika ofisi zake zote zilizopo hapa nchini
ili kuendelea kujipatia elimu juu ya udhibiti wa matumizi salama ya mionzi na
uhamasishaji, uendelezaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia hapa
nchini.
Imetolewa na;
Kitengo
cha Mawasiliano
Tume ya
Nguvu za Atomiki Tanzania
No comments:
Post a Comment