Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
WANAUME nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima tezi dume ili watakaobainika na ugonjwa huo wapatiwe matibabu.
Wito huo umetolewa na Mfamasia Abel Mdemu kutoka taasisi ya Taifa ya Magojwa ya Binadamu (NIMR) ambapo pia alisema tayari NIMR imeshaanza kutoa dawa ya persivin ambayo inatibu ugojwa huo wa tezi dume.
Akizungumza
banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) lililopo katika
viwanja vya maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara maarufu kama
sabasaba, Mdemu amesema tayari dawa hiyo imeshawatibia wagojwa wengi
Amesema
dawa hiyo imepatikana kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo
baada ya kuona wanaume wengi wanapata changamoto ya maradhi.
"Nitoe wito kwa wanaume kujitokeza kupima tezi dume, tayari tumeshapata dawa ya kuutibu ugonjwa huu," amesema.
Ameongeza kuwa, dawa hiyo ni ya asili ambayo imetengenezwa na mimea ya aina tofauti.
"Mimea
ni dawa tezi dume inatibika kwa kwa kutumia mimea iliyopo nchini Ni
vyema kujitokeza kwa ajili ya kpima na kupata matibabu haya"alisema
Mdemu
Amebainisha kuwa, hivi sasa serikali ipo katika mchakato wa kununua mashine kwa ajili ya kuongeza uzalishaji mwingi zaidi.
No comments:
Post a Comment