Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Umma, Dk. Arnold Towo, akimkaribisha Naibu Waziri wa Elimu Mhe. William Ole Nasha, kwa kumuonyesha kombe alipofanya ziara katika Banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam kujionea tafiti zilizofanywa na wataalamu pamoja na wanafunzi wakati wa maonesho ya 43 ya SabaSaba tarehe 3 Julai, 2019.
Naibu Waziri akipata maelezo.
Dk. Aviti John Mmochi kutoka Taasisi ya Sayansi ya Bahari akimpa maelezo Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha, alipotembelea banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akipata maelezo kutoka kwa Safia
Hashimu Makame mjasiriamali aliyenufaika na mojawapo ya tafiti ya Kilimo cha
mwani iliyofanywa na Chuo Kikuu Dar es Salaam kutoka katika Taasisi ya Sayansi
za Bahari iliyopo Zanzibar katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) sabasaba.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akiwa katika banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam akipata maelezo kuhusu tafiti mbalimbali.
Mmoja
wa washiriki wa Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia katika banda
la Chuo Kikuu Dar es Salaam kuhusu tafiti walizofanya.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametembelea banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam tarehe 3 Julai, 2019 katika Maonesho ya 43 ya SabaSaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri alipita na kupata maelezo kutoka kwa watafiti mbalimbali akiwemo Dr. Aviti John Mmochi Kutoka Taasisi ya Sayansi
za Bahari ya Chuo Kikuu Dar es Salaam kilichopo Zanzibar ambaye alielezea zao
la Mwani ambalo mradi huo ulianzishwa na Prof Keto Mshigeni aliyekuwa Idara ya
Mimea ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kusambaza kilimo cha mwani Zanzibar
na Bara, kuendeleza utafiti na kuratibu maendeleo yake.
Kilimo cha mwani kina wakulima zaidi ya 24000 ambao asilimia 80 mpaka 90
ni wanawake. Kwa kuzingatia kuwa bei ya mwani ya shillingi 500 ni ndogo,
taasisi pia imesaidia kuanzishwa taratibu za kuongezea thamani na hivi sasa
kuna bidhaa nyingi zikiwemo za chakula na vinywaji, vipodozi n.k.
vinavyotenezwa na vikundi vya wanawake.
No comments:
Post a Comment