HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2019

MASHINDANO GOLF WANAWAKE TANZANIA YAANZA KUTIMUA VUMBI RC AZINDUA

Mkuu wa Mkoa anogesha ufunguzi
 
Na Mwandishi Wetu

Mashindano ya mchezo wa Golf  kitaifa yameanza kutimua vumbi rasmi jana viunga vya TPC golf club, Mkuu wa mkoa huo akinogesha uzinduzi huo
Mashindano hayo ya kitaifa yanayojumuisha washindani wa mchezo huo kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania yanayoandaliwa na  Chama cha gofu cha wanawake Tanzania TLGU yalianza kutimua vumbi rasmi jana huku washindani wakitamba kuinuka na ushindi huo.
Wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa mkoa huo Anna Mngwira amesifia uandalizi wa mashindano hayo huku akiwataka washiriki wa mashindano hayo kuhakikisha hawajaja kushiriki bali kuondoka na ubingwa wa mashindano hayo makubwa, zaid sana amewaasa washiriki wanayoliwakilisha Taifa kutamba mbele ya wageni Kenya na Uganda.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Golf cha Wanawake Tanzania  Sophia Vigo amesema mashindano ya mefanikiwa kutokan ana amwitikio wa Wqachezaji kutoka maeneo mbalimbali nchini na Nje ya Tanzania.
Ameelezea mafanikio ya mashindano hayo ni mwendelezo wa mafanikio  waliyopata na timu ya Taifa ya Wanawake  nchini Ghana ambapo mshindi wa jumla alitoka Tanzania akihusisha na mashindano hayo makubwa yaliyowezesha kupata timu bora.
Aliongezea kwa kuwaomba wadau wa michezo Tanzania kuwaunga mkono ili kukabiliana na changamoto zao ikiwemo upungufu wa fedha wakati wa uandaaji wa mashindano hayo.
Msimu huu mashindano hayo makubwa ya kitaifa yamejumuisha zaidi ya washindani 50 wa ndani na nje ya Tanzania, yakitarajiwa kupigwa kwa siku tatu mfululizo kabla ya hitimisho lake jumapili hii ambapo bingwa atatangazwa.

No comments:

Post a Comment

Pages