Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wadau mbalimbali kutoka Bodi ya Usajili Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB) Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na wadau wa Sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua mkutano huo
wa Mwaka wa Mashauriano katika Bodi na Taasisi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wadau mbalimbali kutoka
Bodi ya Usajili Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB) Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na wadau wa
Sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua mkutano huo wa Mwaka wa Mashauriano
katika Bodi na Taasisi hiyo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wadau mbalimbali kutoka Bodi ya Usajili Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB) Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na wadau wa Sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua mkutano huo
wa Mwaka wa Mashauriano katika Bodi na Taasisi hiyo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
vifaa mbalimbali vya Mabomba ya Maji katika viwanja vya Diamond Jubilee mara
baada ya kufungua mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa AQRB,CRB,ERB pamoja na
Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
vifaa mbalimbali vya Mabomba ya Maji katika viwanja vya Diamond Jubilee mara
baada ya kufungua mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa AQRB,CRB,ERB pamoja na
Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
moja wapo ya gari linalotumika katika ujenzi wa Miondombimbu mbalimbali katika
viwanja vya Diamond Jubilee mara baada ya kufungua mkutano wa Mashauriano wa
Mwaka wa AQRB,CRB,ERB pamoja na Wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
vitasa mbalimbali vya Milango wakati alipopita kukagua mabanda katika maonesho
ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mchungaji Daniel Mgogo mara baada ya kufungua mkutano huo wa
Mashauriano uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Charles Kitwanga Mbunge wa Misungwi mara baada ya kukagua mabanda katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi
yaliyopo katika viwanja vya Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli amefungua mkutano wa mashauriano wa wadau wa sekta ya ujenzi
hapa nchini na kuwahakikishia Wakandarasi, Wahandisi, Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti za
kuwajengea uwezo wa kutekeleza miradi mingi na mikubwa hapa nchini.
Mkutano huo wa siku 2 umefunguliwa leo tarehe 04 Septemba,
2019 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
wajumbe 4,390 kutoka Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa
Wahandisi (ERB),
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) na Wadau wa huduma za bidhaa
za ujenzi chini ya kauli mbiu “Wajibu wa wadau wa sekta ya ujenzi katika
kufikia uchumi wa viwanda endelevu kwa ustawi wa jamii”.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli amesema katika
kutekeleza sheria inayotaka miradi yenye thamani ya chini ya shilingi Bilioni 10
kutolewa kwa Wakandarasi wa ndani, katika mwaka uliopita miradi 1,068 yenye
thamani ya shilingi Bilioni 267.7 iliyotolewa na Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini (TARURA)
ilitekelezwa na Wakandarasi wa ndani na kwamba mwaka huu Serikali imetenga
fedha nyingine shilingi Bilioni 278.13 kupitia TARURA ambazo miradi yake itatekelezwa
na Wakandarasi wa ndani.
Amesema pamoja na kuwapa Wakandarasi wa ndani miradi
mikubwa mfano ujenzi wa barabara ya lami ya Rudewa – Kilosa, Urambo – Kaliua na
Kimara – Kibaha, Serikali imelipa madeni ya wakandarasi ambapo katika mwaka
2016/17 zimelipwa shilingi Bilioni 557 na mwaka 2017/18 zimelipwa shilingi
Bilioni 833.65.
Ameongeza kuwa kampuni za Wakandarasi wa ndani
zimeendelea kupata kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya maji ambapo
katika mwaka uliopita zimepata miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 386.34
na kwa upande wa miradi ya nishati ya umeme zimepata miradi yenye thamani ya
shilingi Bilioni 996.
“Tunafanya
hivyo ili kuimarisha uwezo wa wataalamu wetu na kampuni za hapa nchini, na pia kwa
lengo la kuhakikisha fedha zetu zinabaki nchini ili zisaidie kuimarisha uchumi
wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli amewakosoa Wakandarasi
na Wahandisi hao kwa vitendo vyao vya kutoshirikiana katika utekelezaji wa
majukumu na miradi, na ametoa wito kwao kujitafakari na kuchukua hatua
zitakazosaidia kuondoa dosari hizo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amezitaka kampuni za
ukandarasi kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, taratibu na uadilifu wa
taaluma yao ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa na upangaji wa gharama
kubwa za miradi huku akitolea mfano wa uamuzi wa Serikali kujenga majengo yake
bila kutumia wakandarasi ili kuokoa fedha nyingi.
“Serikali
imejenga vituo vya afya 352 kwa shilingi Bilioni 184, endapo ujenzi huo
ungefanywa na Wakandarasi tungetumia shilingi Trilioni 1, ujenzi wa darasa 1
umetumia shilingi Milioni 20 lakini tungetumia Wakandarasi tungejenga kwa
shilingi Milioni 50 hadi 60, halikadhalika ujenzi wa bweni bila Wakandarasi umegharimu
shilingi Milioni 75 tena likiwa na fenicha lakini tungetumia Wakandarasi
tungetumia shilingi Milioni 170, sasa kwa gharama kubwa kama hizi ni lazima
mjitathmini na mjirekebishe” amesisitiza Mhe. Rais
Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Wakandarasi hao kuacha
kulalamika na badala yake kutumia fursa ya uwepo wa miradi mbalimbali
inayotekelezwa hapa nchi kuomba kazi na kuzifanya vizuri na amewahakikishia
kuwa changamoto mbalimbali ambazo wameomba zitatuliwe, Serikali itazifanyia
kazi.
Ametoa wito kwa taasisi za elimu kuongeza fursa za
mafunzo kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ambao amesema idadi yao ni ndogo
(chini ya 2,000) ikilinganishwa na idadi ya Watanzania zaidi ya Milioni 50 huku
akiwataka Watanzania kuwatumia wataalamu hao katika ujenzi badala ya kujenga
holela.
Wenyeviti wa Bodi za CRB, ERB, AQRB pamoja na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa namna
anavyotilia mkazo ujenzi wa miundombinu mikubwa ambayo ni nguzo muhimu ya
uchumi hasa tunapoelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda na wameahidi
kumuunga mkono katika jitihada hizo.
Baada ya ufunguzi wa mkutano huo Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa tangazo rasmi la
Serikali kuwa Ndege ya Tanzania aina ya Airbus 220-300 iliyokuwa ikishikiliwa
nchini Afrika Kusini kwa agizo la Mahakama imeachiwa.
No comments:
Post a Comment