HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2019

Serikali Kusomesha Madaktari Bingwa 365 kwa Ajili ya Kusambazwa Maeneo yenye Uhaba

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai akitoa taarifa ya kuanza kutumia mfumo wa Tehama badala mfumo wa makaratasi katika kuwasilisha orodha ya shughuli za bunge wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma. (Picha na Maelezo).

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma

Jumla ya madaktari bingwa 365 wanatarajia kuhitimu mafunzo kuanzia mwaka wa wasomo 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022 ambao watasambazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini kulingana na uwiano wa wataalamu waliopo pamoja na kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sonia Jumaa Magogo juu ya mkakati wa Serikali wa kuongeza Madaktari Bingwa nchini.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Jumanne Miraji Mtaturu akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.

"Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa katika ngazi mbalimbali za huduma nchini ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili," amesema Dkt. Ndugulile.
Ameendelea kusema kuwa katika mwaka 2017/2018, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2 zilizotumika kwa ajili ya kusomesha madaktari bingwa 125 wa fani za kipaumbele katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambao wanatarajia kumaliza 2020/2021.

Aidha, katika mwaka 2018/2019, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 ili kuendelea kugharamia mafunzo ngazi ya kibingwa katika kada mbalimbali za afya 127 katika Chuo cha MUHAS. Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Jumanne Miraji Mtaturu akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kula kiapo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kutoka kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adeladus Kilangi.[/caption] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) wakifurahia jambo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile akijibu swali wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo walipokuwa akijibu swali katika Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Mhe. Mussa Hassan Zungu akiwasilisha Azimio la Bunge la kupmpongeza Mhe. Rasi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo wakati wa Mkutano wa 16, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Boniphace Simbachawene (aliyesimama) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Ofisi hiyo, Januari Makamba (wa pili kushoto), walipokutana katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kulia ni Mbunge wa Kibaha, Sylivester Koka. Mbunge wa Singida Mashariki, Jumanne Mtaturu, akiuliza swali la nyongeza wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo Septemba 3, 2019 jijini Dodoma. Mbunge huyo ameapishwa leo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika kutokana na nafasi kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kukosa sifa ya kuendelea na Ubunge. Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki waliomsindikiza Mbunge wao, Jumanne Mtaturu, kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake wakipunga mikono baada ya kutambulishwa Bungeni katika Mkutano wa 16 wa Bunge kikao cha kwanza leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mtaturu amesindikizwa na zaidi ya wananchi 200 kutoka jimboni kwake. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO).

Dkt. Faustine amesema, katika mwaka 2019/2020, Wizara imetenga jumla ya shilingi 1,844,617,090 kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya wataalamu bingwa katika fani za vipaumbele.

"Kutokana na uhaba uliopo kwenye hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara itahakikisha fedha hii inatumika vyema katika kusomesha wataalamu wanaotoka kwenye maeneo yenye uhaba mkubwa," amesema Dkt. Ndugulile.
Aidha, wizara kupitia hospitali za rufaa ngazi ya Taifa na Taasisi za nje zitaendelea kuendesha kambi za udaktari bingwa hapa nchini, kwa lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalamu.

No comments:

Post a Comment

Pages