NA SALEIMAN MSUYA
WAZIRI
wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewaoamba wafanyabiashara
wa Kitanzania kushiriki katika Kongamano la Kwanza la Biashara na
Uwekezaji ili kukuza biashara baina ya nchi hizo.
Kongamano
hilo na maonesho ya bidhaa na huduma lifunguliwa na Rais John Magufuli
na Rais Yoweri Museven Septemba 6 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa
wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Alisema wafanyabiashara wa Tanzania wanapaswa kutumia fursa zilizopo nchini ili kuwavutia wenzao wa Uganda.
"Kongamano
hili linaloshirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda ni la
kwanza kufanyika nawaomba wafanyabiashara na wananchi wajitokeze kwa
kujisajili," alisema.
Waziri
Bashungwa alisema Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa mbalimbali za mazao na
vifaa nchini Uganda hivyo kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi.
"Hii ni fursa kwetu Watanzania tunapaswa kuitumia ili kuweza kunufaika nayo kibishara na kiuchumi," alisema.
No comments:
Post a Comment