HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2019

TMA YAZINDULIWA RASMI KUWA MAMLAKA KAMILI YA HALI YA HEWA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi, akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kwenye uzinduzi rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), jijini Dar es Salaam Septemba 5, 2019.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisalimiana na Mkurugenzi Huduma za Utabiri, Dk. Hamza Kabelwa.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za Ufundi Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), D. Pascal Waniha, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, jinsi kifaa cha uhakiki wa vifaa vya kupima upepo unafanyika hapa hapa nchini pamoja na vifaa vinavyopima mgandamizo wa hewa pamoja na joto visivyotumia zebaki.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo mara baada ya kupata maelezo ya jinsi kifaa cha uhakiki wa vifaa vya kupima upepo unavyofanyika hapa hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi, akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa uliofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 5, 2019.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), jijini Dar es Salaam.
Ufafanuzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizundua rasmi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi na kulia ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhan Nyenzi.

Igizo kuhusu hali ya hewa.
Ofisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa akiigiza akiwa kazini.
Uzinduzi wa mifumo ya hali ya hewa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA anayemaliza muda wake, Dk. Buruhan Nyenzi, akipokea cheti cha kutambua mchango wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi.

No comments:

Post a Comment

Pages