HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2019

VIONGOZI WA CCM MISENYI KUMSAIDIA MTOTO PACHA KIFAA CHA KUSAGIA CHAKULA

Katibu wa CCM wilayani, Misenyi mkoani Kagera, Hassan Moshi akiwa na Katibu Jumuiya wa Wazazi, Bi. Rehema Mtawala.

Lydia Lugakila, Kagera

Viongozi wa CCM wilayani Misenyi mkoani Kagera wameahidi kununua (BRENDA) kifaa cha Kusagia chakula cha mtoto Pacha Merrynes Benatus mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 aliyetenganishwa na mwenzake Anisia Benatus aliyefariki Dunia wakati akitoka kwenye Matibabu nchini Saudi Arabia.

Viongozi hao wametoa ahadi hiyo wakati wakiwa katika kituo cha Afya cha St. Therese kilichopo katika kata ya Mushasha wilayani Misenyi Mkoani Kagera wakati wakimjulia hali mtoto huyo anayeendelea na Matibabu katika kituo hicho.

Awali Mama wa mtoto huyo Bi Jonesia Jovitus amesema licha ya hali ya mtoto Merrynes kuendelea kuimalika kutokana na juhudi za wahudumu wa kituo hicho kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali ya muhimbili pamoja na Saudi Arabia lakini changamoto kubwa ni kifaa cha kusagia chakula cha mtoto huyo ambapo mama huyo amewaambia viongozi hao kuwa amekuwa akitwanga chakula hicho kutokana na ukosefu wa kifaa hicho(BRENDA)

Kufuati hali hiyo Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Misenyi mkoani hapa Hassani Moshi ameahidi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kukamilisha upatikanaji wa kifaa hicho ili mtoto huyo aweze kupata chakula chenye hadhi inayokubalika,

‘’Hiyo kazi sisi kama chama tutuifanya Ccm kazi yake sio kutafuta kura jukumu letu pia ni kushiriki katika shida na raha za wananchi kwa ujumla kwahiyo mimi naahaidi tutanunua Brenda hiyo na tungejua tungekuja nayo tulishindwa kujua tuje na nini kutokana na masharti ya mahitaji ya mtoto huyu ‘’alisema.

Akitaja vyakula anavyovitumia mtoto Merrynes mama mzazi wa mtoto huyo amesema ni pamoja na Wali, uliosagwa nyama ya kuku wa kienyeji ,karoti vilivyosagwa huku hali mtoto huyo akiwa haruhusiwi kutumia chumvi , sukari wala mafuta ya kula.

Mama huyo amewashukuru viongozi hao kwa kujitolea kununua kifaa hicho kwani amekuwa akipata adha kubwa katika kutengeneza na kuandaa chakula cha mwanae tangu awepo katika kituo hicho huku akiiomba serikali pamoja na jamii kwa ujumla kumsaidia kuboresha nyumba yake kwa kumuwekea umeme na kuisakafu nyumba hiyo , ili mtoto huyo aendelee kukua vizuri kwa kupata mwanga na kukw katika nyumba isiyokuwa na vumbi

Mganga mfawidhi wa kitu hicho Francisca Francis, amewashukuru viongozi hao wa chama cha mapinduzi CCM huku akifurahishwa na ushirikiano mzuri uliopo wa kumhudumia mtoto huyo kati ya madaktari kutoka Saudi Arabia na hospitali ya taifa ya mhimbili wanaohakikisha mtoto huyo anaendelea vizuri kiafya.

Muuguzi mwangalizi wa mtoto huyo Dina Kajuna amesema wanaendelea kufuata masharti ya wataalam wa afya kutoka ndani na nje ya nchi na kufurahishwa na wadau mbalimbali wanaofika kituoni hapo kumfariji mama na mtoto huyo.

Aidha Bi Kajuna amewapongeza viongozi wa chama cha mapinduzi ccm wilayani Wilayani misenyi na ametoa wito kwa jamii kuachana na suala la kupenda kuchangia sherehe za harusi kuliko watu wenye shida na raha

Mtoto Merrynes Benatus na mwenzake Anisia walizaliwa kituoni hapo January 29, 2018 wakiwa wameungana na baadae Pacha huyo kufariki Dunia baada ya kuanza kutapika akiwa kwenye usafiri wa ndege ambapo hali ilibadilika na kusababisha tumbo kuanza kuvimba ndo akafanyiwa upasuaji kuangaliwa tatizo ambapo hali ilibadilika na kusababisha umauti wake.

No comments:

Post a Comment

Pages