HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2019

Vituo vya kupigia kura vyaongezeka Kagera kutoka 1665 mwaka 2015 hadi 1678 mwaka 2020

Kamishna wa Tume ya  Uchaguzi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi mkoani Kagera Bi. Asina Omari, wakati akifungua mkutano huo.


Na Alodia Dominick, Bukoba

Mkoa wa Kagera unatarajia kuwa na vituo vipatavyo 1678 vya kujiandikisha kupiga kura za uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais utakaofanyika mwaka 2020.

Takwimu hizo  zimetolewa  na Kamishna wa Tume ya uchaguzi nchini ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Asina Omari katika mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika  manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Omari ameeleza, katika uchaguzi wa mwaka 2015 vituo vya kujiandikisha kupiga kura vilikuwa  1665 na kuwa katika uhakiki wa vituo uliofanyika mwaka 2018 vituo viliongezeka na kuwa 1678 mkoa wa Kagera huku Tanzania bara mwaka 2015 vilikuwa vituo 36,549 katika uhakiki uliofanyika mwaka 2018 viliongezeka na kuwa vituo 37,407

Ameongeza kwamba uboreshaji wa daftari kwa Kagera utakuwa wa siku saba kuanzia octoba 2 hadi octoba 8 mwaka huu.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi idara ya habari na Tehama Frank Mhando amezitaja sifa za wale wanaopashwa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuwa, ni wale walipoteza vitambulisho vyao, raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 na watakao kuwa wamekamilisha umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi mwaka 2020, waliohama na waliopoteza kadi au kuharibika.

Aidha amewataka waliofiwa na ndugu na jamaa zao kufika vituoni kuwatolea taarifa ili waondolewe kwenye daftari la mpiga kura.

Mmoja wa wadau waliohudhuria mkutano huo, Konchesta Rwamulaza,  amesema kuwa Tume haijatenda haki kutoa siku saba kwa mawakala wa vyama vya siasa kuwa wamepeleka majina yao kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo kabla ya zoezi kuanza la kuboresha daftari kwa kuwa ni muda mfupi.

No comments:

Post a Comment

Pages