HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2019

WAHUJUMU WA MIRADI YA SERIKALI KYERWA KUKIONA

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Rashid Mwaimu akiwa ofisini kwake.

Na Alodia Dominick, Kyerwa

Mkuu  wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Rashid Mwaimu, amesema atahakikisha analinda na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoletwa na serikali wilayani  humo.

Mkuu huyo wa Wilaya Mwaimu ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa ofisini kwake akiongea na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo  wilayani hapo .

Amesema kuwa atapambana vikali usiku na mchana ili kuhakikisha anakomesha watu wanaotaka  kuhujumu miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa  wananchi itolewayo na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania na  kuwa yupo tayari kukesha katika maeneo yote ya miradi ili wananchi  waweze kunufaika na miradi hiyo.

Ameongeza kutokana na jitihada, nguvu na busara za Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika utekelezaji wa miradi ya  maendeleo yeye kama mkuu wa wilaya hatomfumbia macho mtu yeyote anayepanga kuhujumu miradi hiyo.

‘’Sasa Nawaahidi miradi yote inayoletwa na serikali kwa ajili ya wilaya ya Kyerwa nitaisimamia na kuilinda kwa nguvu zote, nitahakikisha adui yeyote haisogelei miradi hiyo ,miradi ni mali ya wananchi ole wenu mlozoea kuitafuna muda umekwisha nitacheza na nyie usiku kucha. ‘’ Alisema Mwaimu .

Hata hivyo amewata wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahimiza  kutowachagua viongozi wabishi, badala yake wachague viongozi ambao ni wazalendo na waadilifu watakao waletea maendeleo.

Katika suala la ulinzi na usalama  wilaya yake ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo amewataka wananchi kuripoti katika vyombo husika mara moja vinapojitokeza  vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyosababishwa na baadhi ya watu wasio waadilifu hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

No comments:

Post a Comment

Pages