NA MWANDISHI WETU
WATAFITI
kutokaTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Taasisi ya Dawa Asili (ITM) wamesema
wakati umefika kwa Serikali kuwekeza katika tafiti za dawa asili ili kuweza
kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Watafiti
hao wamesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa
habari ambao walitembelea ITM iliyopo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa Mabaraza ya
Utafiti wa Sayansi, Ubunifu na Teknolojia unaotarajiwa kufanyika Novemba 11
hadi 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam..
Akizungumza
katika mkutano huo Mtafiti Kiongozi wa COSTECH, Dk, Khadija Malima alisema nchi
ya Tanzania imejaliwa rasilimali miti dawa mingi lakini hakuna uwekezaji
uliowekezwa kuhusu kufikia hatua ya kutengenezwa dawa na kutumika.
Dk.
Malima alisema iwapo nguvu itaelekezwa katika uwekezaji wa utafiti wa afya hasa
tafiti ambazo zinasaidia wanadamu ni dhahiri kuwa dhana ya Tanzania ya viwanda
itatimia,” alisema.
“Sasa
tunataka kujiweka sawa katika tafiti za afya hasa zinazomsaidia mwanadamu, ITM imekuwa
mnufaika kwa miradi ya utafiti kutoka COSTECH lakini bado uwekezaji haujafanywa
wa kutosha kwani Tanzania ina miti dawa mingi ila hajatafitiwa,” alisema.
Alisema
haja ya kuwekeza katika eneo hilo ili kuweza kunufaika na maliasili ambazo
Mungu ameipatia Tanzania hata kutengeneza dawa katika hatua fulani ambayo
inaweza kutoa matumaini,” alisema.
Dk.
Malima alisema tafiti nyingi zilikuwa zimejikita kuleta uelewa hivyo ni vema
kubadilika ili kuhakikisha tafiti zinafikia hatua ya dawa ili kuweza
kuunganisha watafiti na wazalishaji ayaani viwanda.
Alisema
matamanio ya COSTECH ni kuona rasilimali zilizopo kupitia wanasayansi
zinabadilisha maisha ya binadamu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
“COSTECH
itahakikisha kuwa inawaunganisha watafiti na wenye viwanda hivyo dawa ambazo
zimegundulika zitaweza kutibu binadamu, kuwa za kiwango cha juu au za kutosha soko
la nchi za Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara,” alisema.
Mkurugenzi
wa Utafiti (COSTECH), Profesa Mohammed Sheikh, alisema majukumu makubwa ya
taasisi yao ni kuratibu na kuendeleza utatifi na ubunifu nchini hivyo mkutano
huo Mabaraza ya Utafiti ni muhimu kwao kwa kuwahamisisha kufanya tafiti zaidi
ili kuweza kunusu wananchi.
Alisema
ITM ni taasisi ambayo wamefanikiwa kuiwezesha katika vipindi tofauti kufanya
tafiti za dawa mbalimbali ambapo kwa asilimia kubwa matokeo yameanza kuonekana
na kwamba mkutano huo utawafungua zaidi.
“Sisi
COSTECH majukumu yetu makubwa ni kutafiti na kuendeleza ubunifu nchini hivyo
ITM ni kipimo sahihi. Lakini katika mkutano huo kutakuwa na mada tatu ambazo ni
kufungua sayansi, kufanya tafiti na ubunifu kuanzia ngazi ya chini na kuachana
na tabia ya kufanya kazi wakiwa ofisini ili kuweza kupata taarifa sahihi,”alisema.
Mkurugenzi
Mkuu wa ITM, Joseph Otieno alisema kwa miaka zaidi ya 40 ya uwepo wa taasisi
hiyo wameweza kudundua miti dawa zaidi ya 12,000 ambapo miti dawa 2,000
zimerikodiwa, 15 zimefanyiwa tafiti na miliwili imeweza kuwa bidhaa.
Alisema
uwekezaji katika sekta hiyo ni muhimu ili kuweza kuchochea ya maendeleo nchini
kwa kuwa miti dawa ni biashara kubwa duniani ambayo inaweza kubadilisha maisha
ya wananchi kiuchumi na kiafya.
“Tanzania
ina miti mingi nchini na kati ya hiyo asilimia 25 imefanyiwa utafiti kwa ajili
ya matumizi ya dawa mbalilimbali na kwamba iwapo wanataka kuunganishwa watakuwa
na pakuanzia.
Otieno
alisema miti dawa nchi inaweza kutumika kutengeza dawa bora kutokana na miti
hiyo bila kuharibu bioniwayi.
No comments:
Post a Comment