SERIKALI
imesema kuna haja ya kupunguza uingizwaji wa magari nchini yaliyotumika
ili kupunguza hewa ya ukaa inayochangia ongezeko la joto duniani.
Aidha
serikali imesema pia kuna haja ya watu kutumia usafiri wa umma na
kuacha matumizi ya magari binafsi kwani na jambo hilo linachangia pia
ongezeko la joto na maradhi mengine.
Hayo
yameelezwa leo Oktoba 8, 2019 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene katika mkutano wa
watafiti na wanasayansi kutoka barani Afrika na nje waliokutana kwa
lengo la kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na athari zake
zilizoanza kujitokeza duniani hasa barani Afrika pamoja na uzinduzi wa
kitabu.
Amesema masuala
ya mabadiliko ya tabianchi kwa sasa ni suala la dunia kwani shughuli
mbalimbali za kiduniani ikiwemo za viwanda kwa ujumla wake zinasababisha
ongezeko la hewa ukaa.
Ameongeza
kuwa, hewa hiyo imepelekea joto kuongezeka duniani hivyo kusababisha
misimu kubadilika ambapo madhara yake kutokea mvua kupita kiasi pamoja
na ukame.
"Kwasasa
tunajaribu kwenda na mabadiliko ni vyema wadau wakashirikiana, na iko
haja hata kufundisha mashuleni juu ya mazingira ya mabadiliko ya
tabianchi. Magari yanazalisha kaboni monoksaidi, ambayo kwa kiasi
kikubwa inaenda kuharibu hozon layer.
"Hivyo
dunia inafikiri katika kuacha kutumia magari yanayochoma Diesel na
kuanza yanayotumia umeme, lakini sisi hapa ndo tunaongoza kwa kuingiza
magari used, kila mtu anatumia gari lake badala ya kutumia usafiri wa
umma kwahiyo iko haja ya kuona kwa mfano kama hapa Dar es Salaam ambapo
kuna wingi wa watu, basi usafiri wa umma ukaboreshwa watu wakatumia
huo," amesema Simbachawene.
Aidha
are sema kama tutakubali ongezeko la nyuzi joto kufikia zaidi ya 2
duniani, kwa Africa itabidi kuongeza gharama kwani dola milioni 530
zitahitajika ili kukadiliana na mabadiliko hayo.
"Na
kwa hali ya uchumi kwa nchi zinazoendelea tunaweza tukashindwa kuwa na
uwezo wa kukabiliana hivyo kusababisha mafaa, na inakadiriwa tukiendelea
na hali ilivyo tukaendelea kuharibu mazingira halisi tuliyoachiwa basi
tutakuwa na mazingira magumu ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za
kijamii kutakuwa yaani kutakuwa na uhaba wa kila kitu katika dunia.
"Kwahiyo
nitoe wito watanzania watunze mazingira, vyanzo vya maji, kuacha kukata
miti ovyo na kutumia nishati mbadala. Kwa hali ilivyo inatakiwa
kuwekeza katika kutunza mazingira ili kupunguza gharama katika
kukabiliana na mabadiliko hayo," amesema Simbachawene.
Naye,
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mabadiliko ya tabianchi na
mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Pius Yanda
alisema alisema utaweza kibaini maeneo mengine barani Afrika ambayo
yatahitaji kufanyiwa utafiti wa mabadiliko ya tabianchi.
Kuhusu
kitabu walichokizindua, alisema kimeandikwa na wanasayansi watanzania
na wa nchi zingine ambacho kimeelezea mabadiliko ya tabianchi hasa
katika ukanda wa bahari na kuangalia athari zake na kuonesha jinsi gani
utawala bora unaweza ikawa mbinu za kupunguza athari za mabadiliko
hayo.
"Ni kitabu ambacho
kinaweza kutumiwa na wapanga sera, wapanga mipango hasa kuhusu uhifadhi
wa mazingira, ni kitabu ambacho tunaweza kujivunia," alisema Profesa
Yanda.
No comments:
Post a Comment