
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeanza maadhimisho ya wiki ya wateja ambapo itaendesha shughuli mbalimbali
ikiwemo kutoa zawadi kwa wafanyakazi na wateja kwa muda wa mwezi mzima.
Mkuu
wa huduma kwa wateja Ngwitika Mwakihesya amesema kuwa katika kipindi
hicho, MultiChoice Tanzania
itakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha kuwasogelea
wateja karibu zaidi na kufahamu kwa kina uzoefu wao wa kupata huduma za
DStv.
‘MultiChoice
inaamini kuwa wafanyakazi na wateja wetu ndiyo nguzo ya ustawi wetu
hivyo katika kipindi
hiki tutahakikisha tunawafikia na kuwasikiliza maoni yao na hili
tunalifanya ili tuweze kuboresha zaidi huduma zetu na kumfanya mteja
ajisikie kuwa yeye kweli ni mfalme” alisema Ngwitika na kuongeza kuwa
zoezi hilo litahusisha kuwazawadia wafanyakazi mbalimbali
pamoja na wateja na pia kuwatembelea wateja wao maeneo mbalimblai ili
kuwasikiliza na kupata maoni yao.
Amesisitiza
kuwa kutokana na uzito huo, zoezi la kutembelea wateja litafanywa kwa
kushirikiana na
uogozi wa kampuni hiyo “Zoezi hili la kuwatembelea wateja litafanywa
kwa kushirikiana na viongozi hivyo hata mkurugenzi mwenyewe na timu yake
ya Menejimenti wataenda kuwatembelea wateja” alisisitiza Ngwitika.
No comments:
Post a Comment