HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 06, 2019

NDITIYE: WANANCHI MKIWASILIANA SERIKALI TUNAPATA HELA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita.

Prisca Ulomi, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha
NIDA na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoani humo.

Wakati akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwa malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma za mawasiliano zinakuwa zenye ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivu mzuri wa mawasiliano kwa kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane
“Serikali tunataka wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapato ambayo yanaendesha shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye.

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida ya mawasiliano kwenye wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato ya Serikali hivyo inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali “tunashida ya mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi,” amefafanua Mkupasi.

Nditiye amemweleza kuwa amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana
wanapenda mtandao wa Vodacom.

Naye Mbunge wa Mbogwe, Agustino Maselle, amekiri kuwa wanapata huduma za mawasiliano za mitandao mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na Isesya.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza

shida ya mtandao huo na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika kusafiri kwenda Ushirombo.

Akijibu malalamiko ya wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato.


 Nditiye amefafanua kuwa sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni moja inatosha na sio lazima kuwa na mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA wafuatilie na kusimamia jambo hilo Katika ziara hiyo, Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na watoa huduma wa kampuni ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment

Pages