HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2019

WADAU WAKUTANA KUKAMILISHA MWONGOZO WA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Mashirika ya TNC pamoja na PELUM-Tanzania imekutana na wadau wa uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini kwa ajili ya kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini (Guideline for participatory village land use planning, administration and management in Tanzania) 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kazi hiyo, M kurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen Nindi amewataka wadau hao kuhakikisha Mwongozo huo unakuja na majibu ya kisayansi katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya tabianchi kwa malengo ya kuwasaidia wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua kikao cha kikao kazi kuhusu  kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, Morogoro, Octoba 2, 2019.
Bw. Peter Lorri, Meneja Uhifadhi nchi kavu kutoka Asasi ya kiraia ya The Nature Conservancy (TNC), akieleza ushiriki wao katika uwezeshaji wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bw. Angolile Rayson Afisa Programu  kutoka PELUM Tanzania akielezea ushiriki wao katika Mwongozo wa mpango wa matumizi ya ardhi na namna walivyoshiriki katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja uandaaji wa matumizi ya ardhi katika baadhi ya vijiji nchini Tanzania
 Bw. Joseph Osena  Kaimu Mkurugenzi, mipango ya matumizi ya ardhi, usimamizi na uratibu akiwapitisha wana kikosi kazi aina 14 za ramani ambazo zinatakiwa kuandaliwa wakati wa upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ambazo zitaifanya mipango hiyo kuwa ya kisayansi zaidi.
Bw. Paulo Tarimo Mkurugenzi wa Mipango ya ya Matumizi ya ardhi Wizara ya Kilimo, akichangia jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bw. Zakaria Faustin Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TNRF akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bi. Albina Burra kutoka  Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) akijibu na kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau katika mjadala wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
 Kikao kazi cha kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, kikiendelea.

No comments:

Post a Comment

Pages