Muonekano
wa baadhi ya madarasa yaliyojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Mhe. Daniel Chongolo katika shule ya sekondari Twiga iliyopo Kaya ya wazo kabla
ya kuzinduliwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na wanafunzi, walimu washule ya Sekondari Twiga
iliyopo Kata ya wazo hili leo, alikuwa akizindua na kukabidhi madarasa kwa
walimu wa shule leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimsikiliza mwananchi
aliyekuwa akimueleza jambo mara baada ya kumaliza kuzindua na kukabidhi
madarasa kwa walimu wa shule ya Sekondari Twiga.
Dar es Salaam, Tanzania
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amekabidhi madarasa sita na ofisi tatu
za walimu katika Shule ya Sekondari Kigogo iliyopo kwenye Kata hiyo pamoja na
Shule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya Wazo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake
wakuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anakosa nafasi ya kusoma kwa changamoto ya
madarasa.
Mhe.
Chongolo amezindua madarasa hayo ikiwa ni katika mpango wake wa kujenga
madarasa 100 kwakushirikiana na wadau mbalimbali wapenda maendeleo katika
Halmshauri hiyo.
Akizungumza katika
uzinduzi huo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa anawapongeza wadau hao walioshirikiana
naye katika ujenzi huo kwani madarasa hayo yatasaidia wanafunzi waliomaliza darasa
la saba kuendelea na masomo ya Sekondari badala ya kukaa nyumba.
Amesema kuwa
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli iliamua kutoa
elimu bure kwa kila mmoja ilikuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayekaa nyumbani
bila kusoma na kwamba atahakikisha
madarasa hayo yanajengwa ilikutimiza adhma hiyo.
Amefafanua
kuwa kutokana na mpango wa elimu bure uliotolewa na Rais Dk. Magufuli kumekuwa
na ongezeko kubwa la watoto wanaosoma hivyo serikali itahakikisha kila mmoja anapata
nafasi ya kusoma wakiwa kwenye vymba vya madarasa.
“ Awali
tulikuwa na changamoto ya walimu lakini Mhe. Rais amehakikisha kuwa changamoto
hiyo imekwisha ,hivi sasa tunachangamoto ya vyumba vya madarasa , hili nalo
litakwisha, niwahakikishie serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi
wake” amesema Mhe. Chongolo.
Nakuongeza kuwa” leo hii nimekuja mwenyewe
kuzindua madarasa haya ili kuona ufanisi uliopo, niseme tu kwamba nimeridhishwa
na nimefurahi kuona madarasa haya yamekamilika, sasa imebaki viti na meza ili
wanafunzi waweze kusoma nanimeambia tayari vimeshaagizwa.
Katika hatua
nyingine Mhe. Chongolo amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza
ndoto zao kwani viongozi wamekuwa wakifanya jitihada zakutosha zakuhakikisha
kwamba wanapata madarasa yakusoma.
Mhe. Chongolo amemtolea mfano Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli kuwa ni kiongozi anayeonyesha
katika kuhakikisha kuwa wanafunzi waliopo kwenye Halmashauri yake wanapata madarasa
yakusomea ili wote waweze kupata elimu bora.
Mhe. Chongolo amesema kuwa “ kazi nzuri
inayofanywa na rais wetu mpendwa ni kuona watu wenye hali ya chini na wale
wenye hali ya juu wanapata elimu sawa, kwahiyo niwasihi sana wanafunzi msome
kwa juhudi kubwa , wekeni juhudi kwenye masomo yenu, ili msingi tunaowajengea hivi sasa uweze
kuimarika.
No comments:
Post a Comment