HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2019

JAMII YATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

 Mwenyekiti bodi ya NHIF akimkabidhi kadi ya bima ya vifurushi  hivyo  mmoja wa wananchi katika uzinduzi huo
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja.
 
Uzinduzi

Na Asha Mwakyonde

JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF), kupitia  vifurushi vilivyopo katika mfuko huo ambavyo vinamwezesha kila mtu kuweza kujiunga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 28,2019,  kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Anne Makinda, wakati wa uzinduzi wa  vifurushi hivyo  amesema kila mtu anaweza kujiunga na kuangalia kinachoendana  mahitaji yake.

Makinda amesema kuwa  ni vema jamii ikafanya kazi ili kuwa na kipaumbeke cha kulipia bima ya Afya na kwamba kwa lengo la kumsaidia pale atakapokuwa amepata maradhi.

"Bima ili iweze kuwa bima lazima ukate ukiwa mzima NHIF haikati kwa wangonjwa hivyo ni vema mtu akakata kabla ya kuugua,"amesema Makinda.

Aidha Makinda amewataka watoa huduma za afya kuziimarisha huduma zao  hasa vituo vya serikali.

"Tuna vituo zaidi ya 8000 nchi nzima hivyo naomba tushirikiane  kwa ukaribu na watoa huduma bila kumwangusha Rais John Magufuli,"amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa NHIF,  Bernard Konga amesema mwamuko wa wanajamii kujiunga na bima hiyo ni mkubwa kwani idadi ni kubwa ya waliojuunga.

"Kwa muda wa siku tatu tukiwa hapa Mnazi Mmoja watu wengi wamejitokeza  na hii tumefanya bila kuwatangazia wanakuja tunawapa elimu wanaelewa,"amesrma Mkurugenzi huyo.

Na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Grace Magembe anesema kuwa changamoto za kutojiunga na mfuko wa bima ni kulipia huduma hapo kwa hapo pindi ntu anapougua.

"Gharama za huduma za matibabu zimekuwa zikipanda mwaka hadi mwaka moja ya kazi ya  Wizara ya afya ni kutunga sera,"amesema Grace.

Amesema vifurushi hivyo kila mwanchi anaweza kuzimudu gharama na kwamba isifike mahali mtu akashindwa kupata matibabu  kwa kushindwa kumudu gharama za vifurushi hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages