HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2019

MKOMBOZI BENKI YAPATA FAIDA YA BIL. 1.2


Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya Mkombozi, Prof. Marcelina Chijoriga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 13, 2019, kuhusu mafanikio ya benki hiyo yaliyopatikana katika kipindi cha robo tatu ya mwaka. (Na Mpiga Picha Wetu).



Na Tatu Mohamed


BENKI ya Biashara ya Mkombozi imepata faida ya Sh. Bilioni 1.2 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka.


Hayo yamebainishwa leo Novemba 13, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Thomas Enock alipokuwa akielezea mafanikio mbalimbali ya benki hiyo katika kipindi cha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake ambapo pamoja na mambo mengine imeweza kufungua matawi 11 katika maeneo mbalimbali.


Amesema faida katika robo ya tatu iliyiopata benki hiyo, imetokana na juhudi zilizofanywa na uongozi wa benki hiyo kwa kushirikiana na bodi yake kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizosababisha benki hiyo kupata hasara katika robo ya kwanza na pili.


Enock amefafanua kuwa, katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, benki hiyo ilipata hasara ya Sh. Milioni 227 na Sh. Milioni 902 katika kipindi cha robo ya pili hatua iliyotokana na uwepo wa sababu mbalimbali ikiwemo ya baadhi ya wakopaji kushindwa kuirejesha mikopo waliyoikopa katika benki hiyo.


Ameongeza kuwa, kutokana na changamoto hiyo, benki iliamua kuunda kikosi kazi cha ukusanyaji wa madeni kilichofanya kazi kwa ufasaha hadi kufanikiwa kufanya vizuri katika robo hii ya tatu.


“Imani yetu kuanzia hapa tutazidi kufanya vizuri ili kuleta matokeo chanya ya utendaji wa benki. Hata hivyo mikakati ya sasa ya benki ni kujiimarisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya utoaji wa huduma za kibenki kupitia mtandao ili kuwafikia wateja wengi zaidi,” amesema Enock.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya benki hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya Mkombozi, Profesa Marcelina Chijoriga pamoja na mambo mbalimbali aliyoyazungumza kuhusu benki hiyo amesema kuna haja ya wananchi kupewa elimu kuhusu mikopo kabla ya kuchukua kutoka benki.


Ameongeza kuwa, hatua hiyon itawawezesha wakopaji hao kuondokana na adha wanazozipata hasa pale wanaposhindwa kuirejesha mikopo hiyo huku akibainisha kuwa sababu watu ya wengi kushindwa kuirejesha mikopo hiyo inatokana na wao kukosa elimu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages