Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino (wa pili kushoto), akimkabidhi matofali Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi, Charles Kabeho, kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Chato. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Batholomeo Manunga. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi ya za mkuu wa wilaya Chato hivi karibuni. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KATIKA
kuunga mkono mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa Soka wa Chato, unaojengwa mjini Chato
mkoani Geita, Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani
ya Sh. Mil. 30.
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni pamoja na mifuko ya saruji 500 na matofali 13,335, huku NMB
ikiahidi kuangalia uwezekano wa kutoa misaada zaidi katika siku za usoni ili
kufanikisha ukamilifu wa ujenzi huo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino, alisema msaada huo ni
uthibitisho wa namna benki yake inavyothamini michezo katika kuimarisha afya ya
watu, hasa vijana.
"Msaada
huu ni sehemu tu ya utaratibu wa kila mwaka wa benki hii katika kuunga mkono
miradi ya maendeleo kupitia Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CRS), ambao
umeifanya NMB kutoa zaidi ya Sh. Mil. 900 hadi sasa kati ya fungu la Sh. Bil. 1
iliyotengwa mwaka huu kusaidia jamii kote nchini," alisema Augustino.
Waakipokea
msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Chato (DC), Charles Kabeho na Mkurugenzi (DED) wa
wilaya hito, Eliud Mwaiteleke, waliishukuru NMB kwa kujitokeza kusaidia
harakati za maendeleo ya michezo wilayani mwao.
DC Kabeho alisema
kuwa, ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya mpango unaolenga kuamsha ari ya maendeleo
ya michezo wilayani humo, sawa na ilivyo miradi mingine ya kimkakati
inayoratibiwa katika wilaya hiyo.
Kwa upande
wake, DED Mwaiteleke alisema ujenzi wa uwanja huo unaokadiriwa kuingiz watazamaji
3,000, utakuwa chachu ya maendeleo ya michezo, na kwamba miamba ya soka nchini
kama Simba, Yanga, Azam FC na wengineo, siku moja watakuja kutumia dimba hilo
watakapokuwa katika safari za mechi za Ligi Kuu.
"Tunatarajia
kuwa wenhyeji wa miamba ya soka kama Simba na Yanga, wakati zitakapoamua kuweka
kambi huku, ama watapotembelea wakati wa mechi za Ligi Kuu. Wito wangu kwa
mashabiki wa soka wilayani Chato, kujiunga na huduma za NMB na kuipa nguvu ya
kutusapoti katika ujenzi wa uwanja huu," alisema Mwaiteleke.
No comments:
Post a Comment