HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2019

MOI KUFANYA UPASUAJI WA UBONGO, MGONGO KWA NJIA YA KISASA

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi, akifungua kongamano la sita la madaktari wa ubongo, mishipa ya fahamu na wanaowahudumia wagonjwa mahututi.

Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) , imeanza kutoa hudama za upasuaji wa  Ubongo na Mgongo kwa  kutumia  mbinu mpya ya kisasa.

Upasuaji huo utatumia  kifaa cha kisasa  (Neuro Monitoring  Machine), cha kuangalia mishipa ya fahamu  wakati wa upasuaji  na baada ya upasuaji  ambao utaleta matokeo makubwa kwa asilimia mia moja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Novemba 11, 2019 katika kongano la kimataifa la mafunzo ya madaktari wa ubongo, mgonho, mishipa ya fahamu  pamoja na wanaowahudumia wagonjwa mahututi,  Mkurigenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Respicious  Boniface alisema konhamano hilo ni muhimu wa Watanzania.

“Mfumo huu mpya   ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini na matumizi yake itatumika wakati wa upasuaji ambapo itakuwa inamonita mishipa ya fahamu na itasaidia kutupa uhakika wa upasuaji kuwa wa uhakika”alisema.

Awali akifungua kongamano hilo ambslo ni la sita kufanyika MOI , Mganga Mkuu Bakari Kambi ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisena serikali  itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi mbalimbali za Afya nchini zenye lengo la kusaidia kuongezeka kwa wataalamu na kurahisishja upatikanaji wa huduma.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia madaktari wa mifupa na upasuaji wa ubongo kupata ujuzi wa mpya kutoka kwa wataalamu wenzao.

“Kongamano hilo lina lengo la kutoa mafunzo ya kuwaongezea ujuzi na weledi kwa wataamu wetu litasaidia kutokana na kukutanisha waataalumu kutoka mataifa mbalimbali ambao wameendelea katika suala zima la huiduma ya upasuaji”alisema

Alisema  baadhi ya  wagonjwa watanufaika kutokana na madaktari hao kurtoka nje watapata nafasi ya kuwafanyia upasuaji.

Aliongeza kuwa   mafunzo hayo yana tija kwa kuwa yanawapatia  wataalumu wa ndani ujuzi na uzoefu ambao utatumiwa hapa nchini.


Alisema serikali imefanya uwekerzaji mkubwa katika Taasisi ya Moi kwa kuwa na vifaa vingi ambavyo vitasaidia wataalumu kutoa matibabu kwa urahisi na haraka.

Pia alisema wizara imejipanga kuja na program maalumu ambayo inakuwa inapam,bana na magonjwa yasiyoambukiza.

“Kama ambavyo kumekuwa na program za kupamabana na magonjwa mbalimbali basi na sasa wizara inakuja na program hiyo ambayo itapambana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo itaanza Disema 14 mwaka huu”alisema

Naye Mtaalam wa upasuajii kutoka Weill Cornell Medicine NewYork, Roger Harti alisema kjongamano hilo litakwenda kuongeza urahisi wa matibabu ya upasuaji kwa wataalamu kutokana na kubadilishana uzoefu.

Kongamano hilo limehudhuriwa na madaktari zaidi ya 100 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Marekani  ambapo limeratibiwa na  kwa ushirikiano  kati ya MOI na Chuo kikuu cha Weill Comell  cha nchini Marekani.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages