Nancy Sumari. |
Na Janeth Jovin
WAZAZI,
walezi na jamii kwa ujumla wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa
kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi ikiwamo ya kupata elimu,
chakula, afya bora, kucheza pamoja na usalama wao wa kuishi.
Hayo
yameelezwa jijini Dar es Salaam leo na mwandishi wa kitabu cha Haki
Nancy Sumari wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuzindua kitabu hicho.
Sumari
alisema anafahamu kuwa sheria na hazi za watoto zipo lakini walio wengi
awazifahamu hivyo ipo haja ya jamii kuzifahamu kwa kina na kuhakikisha
wanazifuata ili kuweza kuwa na kizazi bora cha sasa na baadae.
"Nimeandika
kitabu hiki kwanza kuwasaidia watoto watambue haki zao ili waweze
kuzisimamia na wasinyanyaswe wala kufanyiwa ukatili, lakini pia wazazi,
walezi na jamii kwa ujumla nao wazisome na watambue wajibu wao kwa
watoto.
Kitabu hiki,
kimekamilika na kitauzwa kwa sh. 6000 lakini natambua kuwa wapo watoto
na wazazi ambao hawana uwezo wa kununua hivyo nitakiweka katika maktaba
kuu ya taifa na watakisoma bure kabisa wakienda huko," alisema.
Alisema
ndani ya kitabu hicho cha Haki kuna picha nyingi ambazo zimeambatana na
maneno ambayo yatawasaidia watoto kujifunza zaidi huku wazazi na walezi
kusoma na kuelewa kwa urahisi haki za watoto.
Aidha
alisema anaamini kuwa kitabu hicho kitawafikia watoto wengine na
kuongeza kuwa malengo yao ni kuhakikisha kila mtu anapata fusra ya
kukiona na kukisoma.
"Nimeandaa
kitabu hiki kwa miaka minne mpaka mitano na kimeandakwa kwa lugha ya
Kiswahili kwa kuwa natambua kuwa lugha hii yetu imefikia sasa hadhi ya
kimataifa, hivyo nami anaendelea kukiimarisha kiswahili," alisema.
Aidha
Sumari amewataka wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao wanapata muda wa
kutosho wa kucheza kwani jambo hilo uwajenga zaidi kimwili na kiakili.
"Unajua
wazazi wengi wanafikiria kuwa watoto wakicheza wanapoteza muda jambo
ambalo si kweli hata kidogo, niwaambie kuwa watoto wanaopata muda wa
kucheza wanajengeka kiakili na kimwili," alisema Sumari.
No comments:
Post a Comment