Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.
John Mongella akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58
ya Uhuru wa Tanzania leo Novemba 27, 2019 Jijini Mwanza, maadhimisho hayo
yanafanyika mkoani humo kwa mara ya
kwanza.
Sehemu ya Waandishi wa
Habari wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa
mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella na
waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Novemba 27, 2019 Jijini Mwanza,
maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo
kwa mara ya kwanza.
Na
Mwandishi Wetu, Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya
Jamhuri zinazotarajiwa kufanyika Kitaifa
mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari
Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongella amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika
Disemba 9, 2019 kwa mara ya kwanza katika mkoa huo katika uwanja wa CCM
Kirumba.
Kauli mbiu ya sherehe hizo ni “
Miaka 58 ya Uhuru na miaka57 ya Jamhuri:Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni
Msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa Letu,” Alisistiza Mhe. Mongella.
Akifafanua amesema kuwa Shughuli
zitakazofanyika wakati wa madhimisho hayo ni pamoja na gwaride maalum, burudani
kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya,ngoma za asili kutoka mikoa ya Mwanza,
Kagera na Mara.
Aidha Mhe. Mongella amesema kuwa
kutakuwa na shughuli mbalimbali kuelekea maadhimisho hayo ikiwemo Mashindano ya
ngonjera, Maigizo,Kwaya,Mashairi, Mashindano ya mbio za mitumbwi,Bonanza la
michezo, mchezo wa bao, na mechi ya mpira wa miguu.
Shughuli za kikanda
zitakazofanyika ni pamoja Kongamano la
Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu litakalofanyika tarehe 6, Disemba, 2019 Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.
Alibainisha kuwa baadhi ya
viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hizo ni pamoja na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt. Ali Mohamed Shein.
Viongozi wastaafu wakiwemo Marais,
Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe hizo,Aidha
, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao nchini ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe hizo.
Juma la kilele cha maadhimisho
hayo litakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika kikanda kuanzia Disemba 2,
2019 hadi tarehe 8 Disemba, 2019 kwenye mikoa ya Kagera, Mara, Geita, Simiyu,
Shinyanga na Mwanza.
No comments:
Post a Comment