HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 28, 2019

NCHI SITA KUSHIRIKI MASHINDANO YA GOFU YA TANZANIA OPEN 2019 ARUSHA

Wachezaji wa Gofu 150  wakiwemo kutoka Kenya,Uganda, Malawi, Zambia, Burundi na Rwanda na Wenyeji Tanzania wanatarajia kuingia Viwanjani katika Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Gofu ya Tanzania Open Mwaka 2019 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho (leo) katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania TGU Criss Martin alisema ri maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa mashindano na zawadi Nono ikiwemo ya gari itatolewa.

“ Tuna Zawadi nono na kubwa Zaidi ni Gari aina ya rav 4 ambayo itakwenda kwa Mchezaji atakayefanikiwa kupiga mpira mmoja na kuingiza Shimoni Hole in One” alisema Martin.

Aliongeza kuwa wachezaji wa kulipwa ndio watakaoanza sambamba na Kundi A na kufuatiwa na kundi B na Mashindano yanatarajiwa kumalizika  Jumapili .
Pia alisema mashindano haya hayahusishi Wanawake wala Watoto na makundi ni A na B ambao ndio wanakidhi ushiriki wa Mashindano hayo huku wachezaji wa kulipwa wakoiwa kama wanogeshaji.

Kwa upande wake Mwanakamati wa mashindano hayo Kapteni Japhet Masai alisema Mashindano haya ni ya Gross Mikwaju ya Jumla kwa kujumlisha siku zote.

Aliongeza pia kuwa Sheria zitatumika za Kitaifa ambazo zimeainishwa katika karatasi ya kuandikia matokeo sambamba na sheria za Kimataifa.

Klabu za Tanzania zinazoshiriki mashindano haya yaliyodhaminiwa na Oryx, Super Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam na Serengeti ni Lugalo Gofu Klabu na Dar es Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro Gymkhana, Arusha Gymkhana, Mufindi na Zanzibar sea Cliff na am.

No comments:

Post a Comment

Pages